Mwanangu na Kikwete

Mapinduzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2008
Posts
2,418
Reaction score
98
Majuma matatu kutoka sasa mtoto wangu anayesoma elimu ya chechechea ataadhimisha siku ya kuzaliwa kwake. Kasema mwaka huu hataki zawadi wala keki, anataka aende kumtembelea Raith Kikwete.

Naombeni ushauri wa jinsi ya kumkutanisha mwanangu huyu na Mheshimiwa Kikwete.

Natanguliza shukrani kwa yeyote aliye tayari kunisaidia.
 
Peleka maombi ikulu au subiri wakati mkwere anapita kwenye moja ya mihadhara yake ya kupiga kampeni
 
Ushauri wangu ni kwamba inabidi kumkinga mwanao na matangazo ya biashara yaliyopita kiasi. Mwanao inabidi ajifunze kusoma na kufanya mambo ya kitoto, inaonekana pengine anamlinganisha Kikwete na "action hero figures" kama kina Super Man na Spider Man etc, anajiuliza huyu mtu ambaye yupo kwenye TV kila siku, kila ninapoangalia namuona ni mtu wa aina gani ? Lazima atakuwa si mtu wa kawaida. Inabidi aonyeshwe kwamba Kikwete ni mtu wa kawaida tu, ama sivyo tutatengeneza vikwete wengine wengi sana tu.
 
Mpige jezi ya yanga....ukifika pale plot 1 unakuta lango likiwa wazi linakungoja....
 
Mpige jezi ya yanga....ukifika pale plot 1 unakuta lango likiwa wazi linakungoja....

Anataka kumtembelea raith Kikwete sio kupewa jezi ya yanga. Pia nisingependa kumwambia haiwezekani kabla sijajaribu kutafuta njia ya kumkutanisha na huyo. Kwa mzazi atanielewa namaanisha nini kama ambavyo Kiranga kanielewa.
 
You might be right.
 
Well,
Si unajua huu ni msimu gani?? Maaskari wa magogoni wakiona jezi ya yanga wanachanganyikiwa....try it! :blah::blah:
 
muheshimiwa unayemzungumzia hapa ndo kikwete? Ni kweli uko ofisi moja na kikwete tunayemjua? au umetumika kiasi kwamba unatumia trial and errors kujua baba halisi wa mtoto?

Kama ni ya kweli hayo mi nakushauri nenda hospitali kwanza kamuone daktari bingwa wa watoto, amfanyie mwanao medical check up ili kugundua kama nayeye ana ugonjwa mbaya wa " KUANGUKA ANGUKA". Unajua kuna baadhi ya magonjwa ni ya kurithi?
 
muheshimiwa unayemzungumzia hapa ndo kikwete? Ni kweli uko ofisi moja na kikwete tunayemjua? au umetumika kiasi kwamba unatumia trial and errors kujua baba halisi wa mtoto?

Sivyo unavyofikiria. Mimi na baba watoto tuna mtoto atakayeadhimisha siku yake ya kuzaliwa na anataka siku hiyo amtembelee Kikwete.

Unaweza kunisaidia ni jinsi gani au nitumie utaratibu gani ili huyu mtoto akutane na Kikwete?
 
muheshimiwa unayemzungumzia hapa ndo kikwete? Ni kweli uko ofisi moja na kikwete tunayemjua? au umetumika kiasi kwamba unatumia trial and errors kujua baba halisi wa mtoto?

Pheww!!! Kazi kweli kweli
 
simple, nenda naye kwenye kampeni. atapewa na pipi kule
 
Sivyo unavyofikiria. Mimi na baba watoto tuna mtoto atakayeadhimisha siku yake ya kuzaliwa na anataka siku hiyo amtembelee Kikwete.

Unaweza kunisaidia ni jinsi gani au nitumie utaratibu gani ili huyu mtoto akutane na Kikwete?

OOh sorry sikusoma between lines, si unajua tena Mukulu wa nchi naye ni hajatulia sana?

Ushauri wangu: Mkifanikiwa kupata ruhusa ya mwanao kumuona kikwete, fanya juu chini amuone kwa mbali la sivo mwanao anaweza kupata ugonjwa wa kuanguka anguka, na ukimuanza katika umri mdogo hivo ni hatari sana!
 
Kama malezi yenyewe ndiyo haya basi hatuna haja ya kuwa na watoto... utaomba ushauri hata vitu vilivyo ndani ya uwezo wako??? au wewe na mmeo mazezeta??

Malezi ya mtoto kwa kiasi kikubwa yanaletwa na confidence na decision making za wazazi, sasa kama hata mambo haya tunaulizana sijui tunatengeneza taifa gani, hata siku ya kura utakuja kusema naenda kupiga kura, nambeni ushauri
 
simple, nenda naye kwenye kampeni. atapewa na pipi kule

Okay hivi hiyo can work, nikifika pale nimwombee mtoto nafasi ya kuongea amuulize au kumwambia atakayo. Ntacheck siku hiyo Kikwete atakuwa anafanza kampeni wapi.

Thanks
 
Kama malezi yenyewe ndiyo haya basi hatuna haja ya kuwa na watoto... utaomba ushauri hata vitu vilivyo ndani ya uwezo wako??? au wewe na mmeo mazezeta??

Tumekusikia. Asante na ubarikiwe sana.
 
Nashukuru ka kunielewa. Sidhani kama ni busara kunyanyapaa watu wenye matatizo, wawe wanaanguka kwa bahati mbaya au maradhi.
 
akae barabarani kikwete anapopita,kikwete atampa zawadi ya pipi.................au ataenda kubembea naye jamaica si unajua bembea ni kwa ajili ya watoto lkn babu kikwete anabembea na salma
 
VALUER, SAFARI, KONYAGI FOR YOU ON THE HOUSE UTACHAGUA KATI YA HIZO

The Following User Says Thank You to Acid For This Useful Post:

The Finest (Today)​
 
Tumekusikia. Asante na ubarikiwe sana.

Mwanao ana umri gani hivi?

Nenda pale Lumumba mwone Makamba ata organize tu na unaweza pewa t-shirt, khanga na kofia juu kisha unasafirishwa na mwanao kwenye kampeni kama ni Pemba au Unguja utakula shavu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…