Mwanangu wa miezi 7 ananishangaza

g4cool

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
429
Reaction score
206
Habari wandugu, ni miezi 7 tu iliyopita nilipata mtoto wa kiume na ndio mtoto wangu wa kwanza, sasa tatizo ni kuwa ana toa sana jasho, yan ukimlaza sehemu, baada ya muda unakuta ameshapalowesha kwa jasho, na kama ana usingizi inabidi umbembeleze karibu na feni ili aweze kulala, usiku ni mpaka uwashe feni ndio atalala vizuri, na hataki kufunikwa shuka kabisa, je tunavyoendelea kulala huku tumewasha feni, haiwezi kumdhuru mtoto?? na hii kutoka sana jasho inatokana na nini?? au ni kawaida tu??
 

Kabla ya kuja huku, kwa pediatrician mmeshaenda?

Kama mmeshaenda, mmeambiwa nini?
 
hakuna tatizo hiyo ni afya kwa mtoto hiyo huwatokea watoto wengi
 
Mimi mtoto wangu wa kiume(wa pili kuzaliwa), alikuwa anatoka jasho sana, akiwa na umri kama huyo wa kwako, hakupenda kabisa kufunikwa shuka, mpaka sasa ana miaka 7 bado hapendi kabisa kufunikwa. Ana afya njema kabisa.
 

feni ni mbaya sana kwa mtoto wa umri uo.....jiandaeni kutibu pneumonia
 
Vipi weye mama .. ni diabetic
 
Ahsanteni kwa ushauri, siku ya alhamisi ni siku yake ya klinik, nitakwenda kumuuliza dokta
 

Mtoto wako ananyonya sana?? anakunywa maji sana?? Feni utampa mtoto magojwa ya kifua au tumia feni za maji Nakushauri uwe unamlaza uchi na pumpers ila alfajiri uwe unamfunika endapo wewe ni mkazi wa dar.
 
Achana na Feni zitamletea magonjwa ya nimonia na kifua kisichokoma.
 
I hate pampers...mvalishe nepi ya cotton tuu basi na uhakikishe kipindi cha asubuhi kile unamfunika kwa lazima hata kama hataki na feni sio zuri kifua chake bado huyooo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…