Habari wandugu, ni miezi 7 tu iliyopita nilipata mtoto wa kiume na ndio mtoto wangu wa kwanza, sasa tatizo ni kuwa ana toa sana jasho, yan ukimlaza sehemu, baada ya muda unakuta ameshapalowesha kwa jasho, na kama ana usingizi inabidi umbembeleze karibu na feni ili aweze kulala, usiku ni mpaka uwashe feni ndio atalala vizuri, na hataki kufunikwa shuka kabisa, je tunavyoendelea kulala huku tumewasha feni, haiwezi kumdhuru mtoto?? na hii kutoka sana jasho inatokana na nini?? au ni kawaida tu??