DOKEZO Responded Mwananyamala Hospital iongezewe Madaktari, foleni ni kubwa kumuona daktari

DOKEZO Responded Mwananyamala Hospital iongezewe Madaktari, foleni ni kubwa kumuona daktari

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mwananyamala.jpg
Nipo katika Mwananyamala Hospital na nakutana na changamoto kubwa ya upungufu wa madaktari. Wagonjwa ni wengi sana na foleni ni ndefu kiasi kwamba watu wanazidiwa hadi kwenye mabenchi ya kusubiri.

Nimefika hapa tangu saa mbili asubuhi, lakini hadi kufikia saa 8:20 mchana hatukuwa na uhakika wa kupata nafasi ya kumuona daktari. Hali hii inachosha na inawaumiza wagonjwa wengi wanaohitaji huduma ya haraka.

Tatizo kubwa ni kwamba kuna vyumba viwili tu vinavyotumika kuwaona wagonjwa—chumba namba 3 na 4. Hatimaye nilipata huduma saa kumi na moja kasoro, lakini hali hii inaonesha wazi kuna uhitaji mkubwa wa kuongeza madaktari na kuboresha huduma hospitalini. Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua haraka.
Screenshot 2026-05-22 162958.jpg

Majibu ya Hospitali ~ Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala yafafanua kuhusu uchache wa madaktari
 
Back
Top Bottom