Mwanariadha Alphonce Felix Simbu apokelewa ubalozi wa Tanzania Tokyo

Mwanariadha Alphonce Felix Simbu apokelewa ubalozi wa Tanzania Tokyo

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Ubalozi wa Tanzania - Tokyo, umepokea wanariadha wa Tanzania, Sgt. Alphonce Felix Simbu, Mshindi wa Dunia wa Mbio Ndefu (Marathon) katika Mashindano ya Dunia 2025 yaliyofanyika Tokyo, Japan, pamoja na Cpl. Josephat Joshua Gisemo, wakiwa wameambatana na ujumbe wao.

Mapokezi ya ujumbe huo yalihudhuriwa pia na wawakilishi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Japan (Diaspora), maafisa waandamizi wa Serikali walioko Japan kwa shughuli mbalimbali, pamoja na marafiki wa Tanzania kutoka Japan.

Kwa muda wa saa 2:09:48, Sgt. Simbu aliandika ukurasa wa historia ya Taifa letu, akibeba heshima na hadhi ya Tanzania katika medani ya kimataifa kwa ushindi wake wa kihistoria uliopatikana tarehe 15 Septemba 2025.

Pia Soma: Tokyo, Japan: Alphonce Simbu ashinda Medali ya Dhahabu ya kwanza nchini kwa kushinda mbio za Dunia za Marathoni
1758363894587.png


1758364398570.png
 
Hongera simbu,umeliheshimisha Taifa. Nakutakia afya njema na Amani kwa familia Yako.
 
Back
Top Bottom