Mwanariadha Mjerumani mwenye asili ya Tanzania ashinda dhahabu mashindano ya Olimpiki

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Wakuu Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Malaika Mihambo, amelishindia taifa lake medali ya dhahabu katika mashindano ya michezo ya Olimpiki ya long Jump.

Mwanaridha huyo aliruka urefu wa mita saba ili kuchukua ushindi.

Awali Mihambo alikabiliwa na changamoto kadhaa kabla ya mashindano hayo lakini hatimaye alifanikiwa kuonesha umahiri wake.

Katika fainali ya mchezo huo iliofanyika hii leo Jumanne, bi Malaika hakuonesha ishara zozote za kuibuka mshindi.

Urefu wa mita saba alioruka katika jaribio la sita ulimwezesha kuipatia Ujerumani nishani yake ya kwanza ya dhahabu katika mchezo huo tangu Heike Drechsler aliposhinda mwaka 2000.

Nishani ya fedha ilimwendea mshindi mara nne wa mashindano ya dunia na Olimpiki yaliofanyika mjini London Brittney Reese wa Marekani baada ya kuruka mita 6.97 huku Ese Brume wa Nigeria akijinyakulia medali ya shaba na kuiongezea Afrika idadi ya medali katika michezo hiyo.

Sisi Watanzania Tunafail Wapi Kwenye Hili Jambo?
 
Mkuu kama una orodha ya matokeo ya michezo yote na mataifa yanayoongoza kwa medali mpaka sasa naomba unifae.
 
Tanzania Tanzania!
Nimeumia sana kwa kweli.
Wengine miaka ya 1990s tuliwahi kutengeneza andiko na kuliwasilisha kwa wenye mamlaka,lilihusu jinsi ya kutambua Watanzania "potentials" ambao wapo nnje ya nchi au wenye uraia wa nchi nyingine na kuwatumia "effectively".
Mpaka leo hatujapata majibu.
 
Tunafail kwenye tozo na makato ya wabunge mkuu. Hapo ndo akili zetu zilipo
 
Nchi Zile zile za siku zote..
Washindi, wapinzani na wasindikizaji..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Ila hawa jamaa ni wajanja sana Wana michezo yao inakuwa na medali nyingi sana, mfano kuogelea kila style na medali yake kuna mita 50, 100, 200 etc Jumla kuna michezo 16, wanawake na wanaume hio ni 32 tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…