Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza wakati wa mapokezi ya mwanariadha huyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege KIA, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Alphonce Bandya kwa niaba ya Kamanda wa Polisi pamoja na kumpongeza Mwanariadha huyo kwa kuliletea sifa Jeshi hilo, amesema wataendelea kutoa ushirikiano wakati wote kwa timu hiyo ili ipate mafanikio zaidi.
Kwa upande wake Konstebo Transfora mara baada ya kuwasili katika Uwanja huo wa ndege leo Novemba 19, 2024 na kupokelewa na Maafisa, Wakaguzi na Askari amesema nidhamu pamoja maandalizi mazuri aliyoyafanya ndio msingi wa mafanikio hayo ambapo ameahidi kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine.
Kocha Msaidizi wa Timu hiyo Sajenti Oswald amesema usikivu na nidhamu wakati wa maandalizi katika kambi yao sambamba na kupata ushirikiano wa karibu kutoka kwa Uongozi mzima wa Jeshi la Polisi pindi wanapohitaji ndio chachu ya mafanikio yao.