Mwanariadha wa kike kutoka Nigeria afungiwa miaka 10

Mwanariadha wa kike kutoka Nigeria afungiwa miaka 10

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mkimbiaji wa mbio fupi wa Nigeria, Blessing Okagbare amefungiwa kushiriki mashindano ya riadha kwa miaka 10 kwa kukiuka taratibu za kuzuia matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Kikosi cha kusimamia uaminifu kwa wakiambiaji (AIU) kimesema mwanariadha huyo mwenye miaka 33 amefungiwa kwa miaka mitano kwa matumizi ya dawa mbalimbali zilizopigwa marufuku michezoni na miaka mitano kwa kushindwa kutoa ushirikiano kwenye uchunguzi dhidi yake.

Okagbare alisimamishwa wakati wa mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika kwenye mji mkuu wa Japan, Tokyo kwa kukutwa na vimelea vya dawa za kuongeza nguvu kwenye vipimo vya kawaida kabla ya mashindano.

Mwanariadha huyo ana siku 30 za kukata rufaa kupitia mahakama ya usuluhishi wa michezo ya (CAS) kupinga hukumu hiyo.

okagbare.jpg
 
Ana misuli mikubwa kama mwanaume , just like akina serena na venus , Inaonekana kama michezo mingi ni kwa ajili ya wanaume tu ,
 
Back
Top Bottom