Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari Idtech
Mbona CRDB Bank wapo vizuri sana na wanajibu kwa wakati ,sijajua issue yako kwa undani,ila wacheki kwa kutumia barua pepe "info@crdbbank.co.tz" watakujibu haraka sana na kukupa maelezo yaliyojitosheleza.wachek usihangaike.
Sijui labda jimboni alikokuwa akihudumiaHivi Nimrod Hand yupo inji hii?
Nakutafuta inbox mkuuKwanza pole mkuu. Mimi ni lawyer ila siko Moro.
Kwa uzoefu wangu mabenki mengi huwa yanapuuza mambo kwa wateja wa kawaida mpk pale utakapomu-engage Mwanasheria (Wakili) kwenye jambo lako; hapo ndiyo wanaanza kukuona uko serious.
Hatua ya kwanza ni kuwaandikia DEMAND NOTICE AND AN INTENTION TO SUE (HATI YA MADAI NA KUSUDIO LA KUSHTAKI). Hii ni barua ambayo unaweza kuiandika hata wewe mwenyewe (ingawa ni vema zaidi ikiandikwa na Wakili kwasababu inakua na lugha kali kidogo ya Kisheria).
Ikiwafikia lazima wakutafute kwasababu wanajua kesi ikienda Mahakamani jambo litakuwa kubwa zaidi. Pesa ambayo utamlipa Mwanasheria watakurudishia endapo wakikuita kwa ajili ya settlement.
Hapo kuna hela mkuu, ukimpata Mwasheria smart.
Kimsingi hapo una CAUSE OF ACTION (SABABU YA KUSHTAKI) nzuri tu ya UZEMBE KWA UPANDE WA BENKI.
Njoo PM kwa msaada zaidi, naweza kukuandikia nikai-scan nikakutumia ukanilipa kifuta jasho. Kila la kheri mkuu. Ila narudia tena, pole sana.
Nyie ndio wa hovyo maafisa wenu hasa wa mikopo hovyo sana kuna mchaga flani blanch ya kkoo na mngine fathiri kama sikosei yuko main blanch hao ndio walifanya nifunge acc poor customer service in short wanajiona sana...Karibu Stanbic Bank mteja kwetu ni Almasi
...Pole Sana! Hivi CRDB Bado wanavule Ujinga kwamba KADI ikimezwa na ATM ili kuipata ni lazima Uende Tawi lako! Karne hii ?Mrejeasho.
Hawa wapuuzi wameifungua lisaa moja baada ya hii post.
Tunasafari ndefu kama Watanzia kwa hizi taasisi zetu ambazo full admns ni Watanzania wenyewe. Hatuko committed kwa kazi zetu, huduma zetu ni mbovu mno and no one cares.
Habari wakuu,
Naomba kama wewe ni mwansheria ama una firm ya sheria soma hitaji langu hapa then kama utaona kuna uwezekano wa kushinda kesi basi njoo imbox.
Nilifungua acc ya benk Crdb tawi la Morogoro miaka kama mitano hivi iliyopita kipindi naishi Moro nikiwa na mishe zangu hapo.
Nilihamia Mwanza nikaendelea kuitumia acc hiyo na nilimpa mwajiri wangu acc hiyo salary ikiwa inapitia huko.
Mara ya mwisho nimetoa hela mwezi wa kwanza tareh 30 kwenye ATM bila shida.
Tarehe 02 mwezi huu wa pili nilitaka kutoa hela kwenye ATM ikashindikana na hapo ndo tatizo lilipoanzia. Nilidhani ni tatizo dogo tu lingeweza kusovika kwa tawi lolote lile la hiyo benki.
Niliaenda CRDB Kinyata Mwanza nikawaeleza, wakaangalia acc yangu then wakaniambia wenye kuifungua ni huko Moro, wakaniambia tunawaandikia email kuomba kuifungua. Nikawauliza itakuwa tayari kwa muda gani. Wakadai ni hadi email ijibiwe na hawajui itajibiwa lini. Siku iliyofuata nilienda wakanipa jibu simple, email hajajibiwa.
Nikaona isiwe tabu nikatafuta namba ya huduma kwa wateja ya CRDB nikapa nilivyowapigia wakanipa majibu simple. " Nenda na kitambulisho chako cha NIDA tawi lolote la CRDB lililokaribu yako wakufungulie,". Sasa kwa vile kazini kwangu kuna hiyo benki nikaamua kuwatumia wao.
Wakapiga simu directly kwa branch Manager, simu haikupokelewa wakapiga tena hivyo hivyo, hakupokelewa.
Wakawaandikia compliance wao email wakaweka details za acc yangu wakaniambia nitapigiwa simu na hao compliance. Siku zikaenda no calls.
Nikarudi tena hapo nao wakashangaa kuona tatizo langu halijatatuliwa, wakawapigia Compliance waambiwa tuliaandikia email CRDB Moro waishughulikie, wakaamua kumpigia manager wakiwa wameunga watu watatu.
Baada ya simu kuita kwa muda mrefu manager akapokea, akaelezwa tatizo langu. Manager hakutoa majibu akasema nakuja. Wakasubiri zaidi ya nusu saa manager hakutokea, wakampigia staff wa kawaida wakamweleza tatizo langu, staff akaangalia acc yangu akasema acc imekamilika ila staff aliyeisajili ndo alisahau kuweka details zao za ndani ambazo mimi sijui ni details gani aliacha kuweka. Wakasema huyo staff kwa sasa kahamishiwa Mtwara. Wakamuomba aishughulikie akasema anaifanyia kazi.
Days goes on. Hakuna acc haijafinguliwa, nikarudi tena wakapiga simu. This time response is worse, wanadai aliyeifungua alikuwa intern hakujua vitu vingine vinavyohitajika, staff wa Moro wanashauri kwa vile acc ina matitizo waifute.
Staff wa hapa ofisini akamuuliza unaifutaje acc ya mteja ambayo ina hela zake? Huyo staff aliekuwa anaongea naye akasema basi asubiri wamtafute huyo intern aje aifungue.
Hapo ndo tulipofikia, so far nimekopa kila sehemu, na mwanangu anaumwa ndani sina hata mia mbovu.
Kama wewe ni mwanasheria na umesoma lalamiko langu, na ukaona unaweza kushinda case hii ni inbox. Na ingependeza akawa ni mwanasheria wa Mwanza.
Asante
Equity naona watu wawili watatu wanaips recommendation nzuriDaaah pole sana chief.
Ila endapo technology ya crypto isingeingiliwa na hivi vijamaa kutoka stanford university vinavyojidai vinajua kumbe ovyo tu na mwisho kufanya ionekane kama scam, basi matatizo kama haya tusingekua nayo tena.
Bank za tz wana nyodo za kipuuzi sana, hamna sekta naichukia tz kama banking, ni hvo tu haina mbadala. Natumia equity kutunza hela, siwezi weka bank yyt ya tz, maybe kama ni gateway tu ya kupokea lkn sikalishi hela humo
Ukishaona bank wanakufuata kwako, Ujue tayari wewe ni mtu.Hawa hawa Stanibic wa pale Kinondoni HQ? Mteja kwenu ni mfalme lakini mteja huyo huyo akipatwa na tatizo kidogo tena linatokana na sababu zilizo nnje ya uwezo wake mnamruka kama hamjui? Experience ya rafiki yangu ilinifundisha kitu japokuwa alikuwa mteja wenu mkubwa sana na mwisho wa siku alihamia KCB alikopatiwa msaada.Leo hii amekaa sawa kutwa mnamfuata kumuomba arudi kwenu.
Mtu wa maana kabisaUkishaona bank wanakufuata kwako, Ujue tayari wewe ni mtu.