DAVID Evance Komba ambaye ni Mwanasheria kitaaluma na mzaliwa wa Kijiji cha Lwang’a kata ya Kihorogota tarafa ya Isimani katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, amevunja ukimya na kutangaza nia ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Isimani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba mwaka huu.