Mwan mpambanaji
JF-Expert Member
- Apr 3, 2008
- 482
- 131
Katika hali inayoonyesha kuogopa kasi ya madiwani wa chadema,mwanasheria wa halmashauri ya Arusha Bw Paul Mugasha,ameomba kuhamishwa ghafla,na sasa ataripoti Mwanga kwenye kituo kipya cha kazi.Hivi karibuni diwani mmoja wa chadema wa kata ya Levolosi alimweleza mwanasheria huyo kama mtu hatari kwa halmashauri na akasisitiza kuwa lazima ashughulikiwe kwa kuisababishia halmashauri hasara ya mamilion ya fedha.
Huyu mwanasheria ameingia mikataba mingi ya kifisadi,ukiwamo ule wa soko la kilombero uliovunjwa kwa shinikizo kubwa kutoka kwa diwani huyo wa chadema kata ya Levolosi.mkataba mwingine ni wa car park kati ya Halmashauri na Kilimanjaro printers eneo la stend kuu ya mabasi ,unaokusanywa kwa masaa 24,ilihali halmashauri haipati mgao huo.Kampuni hii ilitishia kumshitaki diwani wa kata ya Levolosi Mh Nanyaro,kwa kuwakataza kukusanya ushuru eneo la stend ya Loliondo,katika sakata hili ndio huyu diwani akamweleza mwanasheria ufisadi wake na kwamba umefika mwisho.