Mwanasheria Mkuu (AG) akata rufaa akiomba Aeshi Hilaly kupitia tiketi ya CCM - korti imrejeshe Bung

Mwanasheria Mkuu (AG) akata rufaa akiomba Aeshi Hilaly kupitia tiketi ya CCM - korti imrejeshe Bung

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amekata rufaa katika Mahakama ya Rufani akiiomba mahakama hiyo imrejeshe bungeni aliyekuwa Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly, kupitia tiketi ya CCM.
Hilaly alivuliwa wadhifa huo na mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga.
Hatua hiyo ilifanywa na aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Bethuel Mmila, April 30 mwaka jana kutokana na kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti hicho katika Uchaguzi Mkuu 2010, kupitia (CHADEMA), Nobert Yamsebo.
Hata hivyo, AG amekata rufaa Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu hiyo ya Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga chini ya hati ya dharura.
Katika hati hiyo ya dharura AG anaiomba Mahakama ya Rufani isikilize mapema rufaa hiyo akibainisha sababu mbili za maombi hayo.
Kwa mujibu wa hati hiyo ya dharura aliyoapwa na wakili wa Serikali Karimu Rashid, AG anadai kuwa tangu mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga ilipotengua matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Hilaly, hadi sasa wananchi wa Sumbawanga hawana uwakilishi bungeni.
AG anadai kuwa kama rufaa hiyo haitasikilizwa na kutolewa uamuzi mapema, wananchi wa Jimbo hilo wataendelea kukosa uwakilishi bungeni.
Katika rufaa hiyo namba 01 ya Mwaka 2013, mbali na AG, ambaye ndiye mrufani wa kwanza, warufani wengine ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Katandala, Justusi Athanasi – (mrufani wa pili) na ARO wa Kata ya Matanga, Vitus Kapufi.


Chanzo cha habari hii ni gazeti la Mwananchi’ Alhamisi, Januari 17,2013
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...faa-ukishindwa-uchaguzi-shitaki-mwenyewe.html

"Bali pia kisheria, kuna kitu ambacho Mahakama ya Rufaa imekifanyia uamuzi.

Nacho ni kwamba kuanzia leo hakuna tena wagombea walioshindwa uchaguzi kujificha nyuma ya wapiga kura kufungua kesi mahakamani.

Mahakama ya Rufaa imesema wazi kuwa ukishindwa uchaguzi shitaki mwenyewe.

Mpiga kura akitaka kushitaki aonyeshe pilipili ambayo hajaila inamwashia nini.
"
 
Back
Top Bottom