...La msingi ni kuhakikisha suala la uhusiano kati ya DPP na AG unawekwa vizuri zaidi.
...Ninapozisoma sheria hizo naweza kuona kuwa DPP ana mamlaka ya kuanzisha au kuamuru kufanyika uchunguzi utaoweza kusababisha mashtaka dhidi ya mtu yeyote yule. Kama DPP angejua hilo, Rais asingetakiwa kuingilia kati na kuamuru uchunguzi wowote ufanyike.
Lakini hiyo ni tafrisi yangu, lakini hakuna mahali ambapo panasema wazi kabisa kuwa AG au DPP ana nguvu ya kuinitiate investigation of a criminal nature kuhusu suala lolote katika Jamhuri yetu. Kama wangekuwa nao hadi sasa hivi tungekuwa na watu wanafuatilia suala la Buhemba, Mwananchi Gold, n.k n.k
Hofu yangu ni kuwa kazi ya DPP imevamiwa na watu wa PCCB.... ambao wamekuwa wakidandia uchunguzi wowote wa kihalifu ili kuona mambo ya rushwa hasa yale yenye high profile. Badala ya kuangalia uwepo wa rushwa kubwa lilitakiwa ni kama kuangalia kuna what is known as "criminal activity" or "acts of criminal nature". Na hili lilitakiwa kufanywa na DPP.
Kwa hiyo nadhani kimsingi tuko pamoja.
Mwnkjj,
To the extent that sio DPP wala AG mwenye nguvu ya kuanzisha uchunguzi anavyotaka, tuko pamoja. Lakini ukisema, kwa tafsiri yako, DPP ana hizo nguvu hapo ndio mimi unanichanganya, kama sio wewe kujipinga.
Unasema kazi ya DPP imevamiwa na PCCB. Kazi ipi hiyo, kuanzisha uchunguzi? Kama ni kuanzisha uchunguzi, ambacho ndicho kilio cha mada yako, hiyo nguvu tumekubaliana hana. Halafu hata angekuwa nayo, nilidhani ulipendekeza nguvu hiyo awe nayo AG. Na kama unakubali awe nayo AG, sasa huyu DPP wa nini?
Mtu mwenye mamlaka -tena mwenye wajibu - wa kuanzisha uchunguzi akisia harufu ya jinai sehemu ni IGP na mapolisi wake wote. (Criminal Procedure Act, 1985, sect. 10 (1)). Lakini IGP hana mamlaka ya mwisho ya kushitaki. DPP anaweza kutengua shitaka lolote bila sababu.
Ndo maana nikashauri nguvu za kushitaki za DPP, na
wajibu wa IGP wa kuanzisha uchunguzi akisikia harufu ya uhalifu sehemu (umekiita hiki kitu "trigger clause"), na nguvu za jumla za AG kama ofisa mkuu wa Sheria nchini, hizi nguvu apewe mtu mmoja. Upacha wa hivi vyeo ni ukiritimba. Vingine vichanganywe. Zaidi ya kuwa ukiritimba, pia ni cofusion ambayo inageuzwa loophole ya ufisadi. Confusion by design: Changa la Macho!
Huwezi kuwa na watekelezaji Sheria ambao mikono yao imefungwa kwa sababu nguvu zao zimemegwa megwa kama vipande vya kashata kati ya Waziri wa Sheria na Katiba, Attorney-General, Director of Public prosecutions, Director of Criminal Investigations, Inspector General of Police, Tume Maalum za Uchunguzi, Tume za ghafla ghafla za Rais, na Executive Orders za Rais anazotoa kwenye viwanja vya wazi: "Nimemwagiza Mwanasheria Mkuu ahakikishe haki inapatikana..."
Hivi vyeo ni vichanganywe!