Mwanasheria Mkuu awe Huru

JokaKuu.. nadhani hiyo ya AG kuwa ni mshauri wa sheria wa serikali ni sehemu tu ya majukumu yake. Kuhusu DCI ni kuwa DCI ni sehemu ya Jeshi la Polisi, ni afisa wa Jeshi la Polisi, hivyo ule Ukurugenzi wake unahusiana na kazi za Polisi au uchunguzi unaofanywa na Polisi. Sijui kama kuna sheria tofauti inayosimamia madaraka ya DCI ukiondoa Police Code. Sijawahi kuiona yawezekana kuwa ipo.
 
Mwanakijiji,

..nadhani masuala yote ya uchunguzi yako chini ya Director of Criminal Investigation.

..labda ungetuelekeza, kwa mifano, ni suala gani ambalo DCI hawezi kulichunguza, na badala yake kazi suala hilo linapaswa kuwa-handled na AG.

..binafsi nafikiri anayepaswa kupewa MAKUCHA zaidi ni DCI. nadhani Ofisi hiyo inapaswa kuimarishwa, na zaidi ningependekeza uteuzi wa DCI uthibitishwe na Bunge.

..Ofisi, na shughuli za Mwanasheria Mkuu, zimejikita zaidi ktk masuala kama miswaada ya sheria, mikataba kati ya serikali na wadau mbalimbali, na utetezi wa serikali mahakamani.

NB:

..Pale wizara ya sheria kuna Katibu Mkuu. Umepata kujiuliza majukumu yake ni yapi?

..Mpaka majuzi, Katibu Mkuu wa Wizara alikuwa the 3rd ranking Officer, baada ya Waziri, na Mwanasheria Mkuu.
 

Mwnkjj,

To the extent that sio DPP wala AG mwenye nguvu ya kuanzisha uchunguzi anavyotaka, tuko pamoja. Lakini ukisema, kwa tafsiri yako, DPP ana hizo nguvu hapo ndio mimi unanichanganya, kama sio wewe kujipinga.

Unasema kazi ya DPP imevamiwa na PCCB. Kazi ipi hiyo, kuanzisha uchunguzi? Kama ni kuanzisha uchunguzi, ambacho ndicho kilio cha mada yako, hiyo nguvu tumekubaliana hana. Halafu hata angekuwa nayo, nilidhani ulipendekeza nguvu hiyo awe nayo AG. Na kama unakubali awe nayo AG, sasa huyu DPP wa nini?

Mtu mwenye mamlaka -tena mwenye wajibu - wa kuanzisha uchunguzi akisia harufu ya jinai sehemu ni IGP na mapolisi wake wote. (Criminal Procedure Act, 1985, sect. 10 (1)). Lakini IGP hana mamlaka ya mwisho ya kushitaki. DPP anaweza kutengua shitaka lolote bila sababu.

Ndo maana nikashauri nguvu za kushitaki za DPP, na wajibu wa IGP wa kuanzisha uchunguzi akisikia harufu ya uhalifu sehemu (umekiita hiki kitu "trigger clause"), na nguvu za jumla za AG kama ofisa mkuu wa Sheria nchini, hizi nguvu apewe mtu mmoja. Upacha wa hivi vyeo ni ukiritimba. Vingine vichanganywe. Zaidi ya kuwa ukiritimba, pia ni cofusion ambayo inageuzwa loophole ya ufisadi. Confusion by design: Changa la Macho!

Huwezi kuwa na watekelezaji Sheria ambao mikono yao imefungwa kwa sababu nguvu zao zimemegwa megwa kama vipande vya kashata kati ya Waziri wa Sheria na Katiba, Attorney-General, Director of Public prosecutions, Director of Criminal Investigations, Inspector General of Police, Tume Maalum za Uchunguzi, Tume za ghafla ghafla za Rais, na Executive Orders za Rais anazotoa kwenye viwanja vya wazi: "Nimemwagiza Mwanasheria Mkuu ahakikishe haki inapatikana..."

Hivi vyeo ni vichanganywe!
 

Jokakuu,

DCI ni mtu mdogo mno. Anaweza akaleta mashitaka halafu DPP akaamua kuyatengulia mbali bila sababu. Anaebidi apewe hizi nguvu za kuamua kuchunguza ni mtu kama DPP au AG.

Na hao makatibu wakuu Sheria na bureaucrat wengine wote wanaweka "kiwingu" cha kisheria. Hawatakiwi kuwepo. Ndo maana nikasema hivi vyeo vingine vifutwe kati ya AG, DPP, DCI, PCCB...na maagizo ya Rais kama vile "Mwanasheria Mkuu ahakikishe Sheria inafatwa..." nayo yakome kwa sababu hatutaki kutegema maagizo pale anapo jisikia Rais.
 
Kuhani Mkuu,

..kama DCI ni mtu mdogo mno basi apewe MAKUCHA ili alingane na wenzake.

..DPP anaweza kufuta mashtaka ikiwa atabaini kwamba ushahidi na vielelezo alivyopewa havimpi uwezo wa kujenga mashtaka, na kuhakikisha hukumu inapatikana. kwa maana nyingine hapo anasema DCI hakumpa msaada mzuri.

..kuna uwezekano pia kukawa na DPP mhuni ambayo atakiuka maadili ya kazi yake na kuamua kufuta mashtaka hata ktk mazingira yasiyostahili.

..hata kama tutafuta vyeo vya DPP au DCI bado hatuwezi kufuta MAJUKUMU/PORTFOLIOS zao. bado watakuwepo watendaji ambao watakuwa wanatekeleza majukumu ya DPP au DCI wa sasa hivi.

..pia labda mnielimishe zaidi katika suala hili, lakini nadhani hata ktk nchi za wenzetu taasisi za uchunguzi ni tofauti na zile za mashtaka.

..kama sikosei kwa nchi kama Marekani wana FBI ambayo inafanya uchunguzi, halafu kuna ofisi ya Federal Prosecutor ambayo inashughulika na mashtaka. vilevile kuna ofisi za Attoney General na Solicitor General.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…