Mwanasheria Mkuu, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi: Tarehe anayozikwa Rais aliyefia madarakani kuwa mapumziko

Mwanasheria Mkuu, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi: Tarehe anayozikwa Rais aliyefia madarakani kuwa mapumziko

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amewasilisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2023 Bungeni Jijini Dodoma ikiwemo Sheria ya Mazishi ya Viongozi wa Kitaifa, Sura ya 419 ambapo pamoja na mambo mengine marekebisho haya yanakusudia kutoa mamlaka kwa Rais kutangaza tarehe ya maziko ya Rais aliyefariki akiwa madarakani kuwa ni siku ya mapumziko.

“Sehemu ya Tano ya Muswada inapendekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mazishi ya Viongozi wa Kitaifa, Sura ya 419 ambapo kifungu cha 6 kinapendekezwa kufutwa na kuandikwa upya kwa lengo la kuboresha masharti kuhusu mamlaka ya Rais kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi wa Kitaifa au Kiongozi mahsusi aliye madarakani”

“Marekebisho hayo pia yanampa mamlaka Kiongozi mahsusi aliye madarakani kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, vilevile marekebisho haya yanakusudia kutoa mamlaka kwa Rais kutangaza tarehe ya maziko ya Rais aliyefariki akiwa madarakani kuwa ni siku ya mapumziko”

“Lengo la mapendekezo haya ni kuweka bayana na kutofautisha mamlaka zinazopaswa kutoa matangazo ya vifo vya Viongozi wa kitaifa na Viongozi mahsusi, vifungu vya 9 na 10 vinapendekezwa kurekebishwa ili kutoa Mamlaka kwa Kiongozi mahsusi aliye madarakani kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, lengo ni kutambua utaratibu unaotumika sasa ambapo pamoja na kwamba Sheria imemtaja Rais kama mamlaka ya kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, matangazo ya aina hiyo kwa kawaida yamekuwa yakitolewa na Viongozi mahsusi walio madarakani”
 
Toka tupate uhuru.miaka zaidi ya 60 ni raisi mmoja tu aliyekufa akiwa madarakani

Sioni shida kwa hilo lipitishwe tu na bunge
Ni kifo kizito sana
Kwa hiyo una hakika kwamba ndivyo itakuwa nyakati zote? Yakitokea ya Zambia utasemaje?

Nasisitiza hii ni aina nyingine ya ujinga.
 
Kwa hiyo una hakika kwamba ndivyo itakuwa nyakati zote? Yakitokea ya Zambia utasemaje?

Nasisitiza hii ni aina nyingine ya ujinga.
Viongozi kufa madarakani ni kitu adimu sana

Pia mfanyakazi aliye ofisini akifa msiba ni wake ni tofauti na mfanyakazi mstaafu

Wa ofisini msiba hubebwa ns ofisi mstaafu akifa wake na familia yake

Tofautisha hivyo vifo havilingani

Mstaafu na aliye madarakani vifo vyao tofauti japo wote wafu
 
Kwa hiyo una hakika kwamba ndivyo itakuwa nyakati zote? Yakitokea ya Zambia utasemaje?

Nasisitiza hii ni aina nyingine ya ujinga.
Mbunge aliyeko madarakani akifa treatment ya msiba wake tofauti na mbunge mstaafu akifa sembuse nafasi ya uraisi
 
Sawa tu wafanye wanavyojua maana vyombo vya ulinzi na usalama navyo vimekuwa vikundi vya kusifu na kuabudu si kushauri tutamiss sana mwamnyange na mabeyo maaana upuuzi unaondelea kutendeka serikalini wakutusaidia sasa hivi ni Jeshi tu si mwanasheria wala mwanasiasa ni jeshi kutoa tamko ngazi husika kuwa a chenille mara moja mambo yenu ya ovyo
 
warekebishe tu , kwamba tupumzike mwezi mzima aliofariki kiongozi
nani anajali
sekta binafsi huwa haipumziki iwe sikukuu au la mnaopumzika ni ninyi waajiriwa wa serikalini kwani hata mkipumzika mwezi nzima mna nini cha maana mnachochangia kwenye uchumi wa nchi zaidi ya kula kodi za sekta binafsi?

Mimi sioni shida kapumzikeni tu hata mwaka sekta binafsi ipumue waache kukimbizwa na maafisa wa serikali kila kona huku kodi,kule Askari wa jiji kukimbiza machinga ,kule kuna matraffic kila hatua chache unapigwa mkono,kule ukienda hospitali ohh mkono mtupu haulambwi toa pesa utilibiwe nk kule ufisadi na kule mikataba mibovu nk kapumzikeni tu hata mwaka after all hamfiki hata laki tano ya population ya watanzania milioni 60 Kwani hata mpumzike Mwaka mna impact gani ?

Nyie mamizigo tu .Nendeni mkapumzike tu kwani mkiwepo.mna nini cha maana mnachoongeza kwenye uchumi?
 
Viongozi kufa madarakani ni kitu adimu sana

Pia mfanyakazi aliye ofisini akifa msiba ni wake ni tofauti na mfanyakazi mstaafu

Wa ofisini msiba hubebwa ns ofisi mstaafu akifa wake na familia yake

Tofautisha hivyo vifo havilingani

Mstaafu na aliye madarakani vifo vyao tofauti japo wote wafu
Sasa la public holiday linatoka wapi?
 
Back
Top Bottom