Mwanasheria Mkuu Marekani aamuru uchunguzi kuhusu upigaji kura

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanasheria Mkuu wa Marekani, William Barr amewaamuru waendesha mashitaka wa Serikali kuanzisha uchunguzi kuhusu dosari za upigaji kura, kwa sababu Rais Donald Trump amedai kuwa alishindwa uchaguzi kutokana na udanganyifu.

Barr, ambaye ni mtetezi wa karibu wa Trump kwa muda mrefu, amesisitiza barua yake kwa wanasheria wa Marekani kote nchini sio ishara ya kuwa Wizara ya Sheria ina ushahidi kwa sasa wa matukio halali ya udanganyifu.

Uchunguzi wa udanganyifu katika upigaji kura kawaida hufanywa na majimbo binafsi, ambayo huweka na kuchunguza kanuni zao za uchaguzi. Amri ya Barr imekuja wakati Trump akipambana kuubatilisha ushindi mwembamba wa mpinzani wake wa Democratic Joe Biden katika majimbo kadhaa muhimu -- Pennsylvania, Nevada, Georgia, na Arizona -- ambayo yalimpa Biden idadi ya kutosha ya kura za wajumbe ili kushinda uchaguzi wa rais kwa ujumla.
 
Trump aendelee na kujeza Golf tu sasa, muda wake wa kuwa Rais wa USA unakaribia kuishia
 
Trump anazidi kuimaliza marekani.
 
Wanafarijikaje Kama yeye mwenyewe kaibiwa na analalamika?
Kwamba hata katika dunia ya ‘waliostaarabika’ unaweza kushindwa uchaguzi ila bado ukakomaa na kutafuta kila namna ya kuendelea kubaki Ikulu

Trump hana evidence ya maana. Kapigwa popular votes na zile za majimbo/electoral votes. Hizo kesi zake ataaibikia kwa mara nyingine tena
 
Game Over. Trump aende tu nyumbani wataalam wa sheria wameshasema kuwa madai yake hayana "Merits".
 
Ni sawa kabisa.Upo ushahidi tosha kwamba Biden amesaidiwa na the Deep State kushinda uchaguzi huo,ili aweze kuwasaidia kuendesha agenda zao za kishetani kwa wanadamu.Wanaotaka kufuatilia jinsi wizi ulivyofanyika mpaka kumuwezesha Biden kushibda uchaguzi huo kwa hila,wafuate link ifuatayo.It is simply mind bogling.Katika link hiyo kuna so many threads,will a lot of evidence.



Upo ushahidi mwingi kwamba Trump kaibiwa kura,mwingine huu hapa👇



 
Popular votes na mahimbo mikula moja. Hakuna kura mbili zinazopigwa hapa bali ni le system to ya winner takes all( Winner of popular votes take all electrol college votes in the electoral constituency .
 
Biden kamshinda Trump kwenye majimbo sita alafu still unalalamika umeibiwa, jamaa sio mstaarabu kabisa
 
Achana na conspiracy theories
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…