TANZIA Mwanasheria Mkuu wa Kwanza Mzalendo na Jaji Mstaafu Mark Bomani afariki dunia

TANZIA Mwanasheria Mkuu wa Kwanza Mzalendo na Jaji Mstaafu Mark Bomani afariki dunia

Thanks bro. Namkumbuka kutoka siku za East Africa FM.

Mshua siku moja alirudi home, alisema ametoka kukaa kikao na Jaji Bomani na Jaji Nyalali, aliwasifia sana kwa uwezo wao.

Tumepoteza mzee wa muhimu sana katika taifa.

Alikua nguli. Lakini naamini hata Mzee wako ni wa kaliba hiyo hiyo. Chembe chembe zinajidhihirisha kwako.
 
John Rupia pia,msukuma na mtanzania wa kwanza Tajiri alietoa pesa zake kumsaidia Julius aende Ulaya kuomba uhuru.
Umenikumbusha huyu mzee..

Watoto wake wawili wa kiume Paul na Stephen Rupia ilhali ni watu wazima kwa sasa wamefanikiwa kukeep low Profile maisha yao yote japokiwa wana maisha mazuri siku zote..
 
Umenikumbusha huyu mzee..

Watoto wake wawili wa kiume Paul na Stephen Rupia ilhali ni watu wazima kwa sasa wamefanikiwa kukeep low Profile maisha yao yote japokiwa wana maisha mazuri siku zote..
Kabisa. Huwezi jua wanamiliki majengo pale mjini kati na Upanga. Hata mwanae wa kike bibi Rhoda (Marehemu)alikuwa low profile sana.
 
Kabisa. Huwezi jua wanamiliki majengo pale mjini kati na Upanga. Hata mwanae wa kike bibi Rhoda (Marehemu)alikuwa low profile sana.
Yaani hawa wasukuma walistaarabika mapema mno;
Pesa ipo halafu hawana majivuno kabisa.

Huko Masaki,Oysterbay,Mikocheni kote ni mansion za maana ila hawana kelele..

Astarehe kwa Amani Bi Rhoda pamoja na Kaka yao mkubwa Albano Rupia hawa walikuwa watu haswa...
 

Habari zilizotufikia ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Tanzania, Jaji Mark Bomani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 11, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mtoto wake amethibitisha kifo hiki. Shughuli za msiba zipo nyumbani kwa Marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

View attachment 1565939
Jaji Mstaafu Mark Bomani enzi za uhai wake akiwa na mkewe wakikata keki katika hafla ndogo ya kusherehekea miaka 50 ya ndoa yao mwaka 2017
View attachment 1568923
--
UPDATE 14-09-2020: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aongoza mazishi
--

WASIFU WAKE KWA UFUPI

Mark Danhi Bomani alizaliwa Januari 2 1932, Bunda, mkoani Mara.

Mark alikuwa kati ya watoto kumi wa Mzee Bomani ndugu zake wengine wakiwa Daniel, Paul, Emma, Francis, Martha, Yona, Washington, Phoebe & Neema.

Mark Bomani alisoma shule ya msingi Mwamanyili, Nassa ambapo baba yake mzazi ndiye alikuwa mwalimu wake. Baada ya kumaliza shule ya Msingi, alijiunga na shule ya Bwiru Boys ambapo alisoma mpaka darasa la 10 na baadae alifaulu kuendelea na masomo ya secondary katika shule mashuhuri ya Tabora Boys. Baada ya kufaulu kidato cha 6, Mark alichaguliwa kwenda chuo cha Makerere College nchini Uganda.

ELIMU:

1953 – 1957B.A (Politics, Economics and History), Makerere University, Uganda

1957 – 1958: Diploma in Social Welfare Policy, Institute of Social Studies, The Hague.

1958 – 1961: Bachelor of Laws (LLB), London University

1961: Barrister -at-Law, Lincoln’s Inn, London

KAZI:

1954: Mwakilishi wa Makerere Student’s Guide kwenye Mkutano wa Kimataifa (International Union of Students Conference), Prague, Czechoslovakia.

1959: Kiongozi wa Umoja wa Wanafunzi wote kutoka Tanganyika (Tanganyika Students Association), Makerere University

1962: Wakili wakujitegemea katika mkoa wa Mwanza

1963: Wakili wa Serikali. Akateuliwa na J.K. Nyerere kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu

Katika kazi ya mwanzo aliyoifanya katika cheo chake kipya ilikuwa ni kusaidiana na Mwanasheria Mkuu Roland Brown kutayarisha nyaraka zote za kisheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

1963: Alishiriki katika utayarishaji wa Mkataba wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (Charter of the African Development Bank), Casablanca, Morocco.

1963: Mjumbe katika ujumbe wa Tanganyika uliokwenda Addis Ababa, Ethiopia kuandaa mkataba wa nchi huru za Afrika (Charter of the Organization of African Unity)

1964: Mjumbe wa Kamati ya Wajumbe wa Nchi za Afrika ya Mashariki iliyoundwa kwa madhumuni ya kuangalia uwezekano wa kuunda Shirikisho la Afrika ya Mashariki

1964: Mjumbe wa Tume ya Rais iliyoundwa ili ipendekeze mfumo mpya wa Kidemokrasia wa Chama kimoja. Mapendekezo ya Tume hiyo ndiyo yaliyokuwa Msingi wa mfumo wa Chama kimoja cha Siasa

1965– 1976: Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza mwananchi. Kati ya mambo ya kwanza aliyoshughulikia nikutafuta majaji na mahakimu kutoka nchi za nje ambao waliajiriwa na serikali ya Tanzania katika kipindi ambapo majaji na mahakimu wengi walikuwa wazungu au wahindi. Kati ya watu aliyowachagua ni pamoja na Telford Georges kutoka Trinidad & Tobago aliyekuwa Jaji Mkuu.

1965: Mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU

1967– 1976: Mjumbe wa Kamati iliyoundwa kwa madhumuni ya kupendekeza mfumo mpya wa ushirikiano kati ya nchi za Afrika ya Mashariki. Hatma yake ilikuwa kuundwa kwa Jumuiya ya Afrka Mashariki (East African Community)

1974: Mshauri wa FRELIMO katika kuandaa Katiba mpya ya Msumbiji na utaratibu wa Serikali yake

1976: Baada ya kuombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais J.K. Nyerere alimruhusu Mark Bomani kujiunga na Utumishi wa Umoja huo kwa madhumuni maalum ya kusaidia katiak matayarisho ya Uhuru wa Namibia.

1976: Naibu Mkurugenzi (Deputy Director), U.N Institute for Namibia, Lusaka, Zambia

1978: Baada ya kuombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuwa mshauri wake wa mambo ya kisheria, Mark Bomani alikwenda Namibia na Afrika ya Kusini kuzungumzia juu ya utaratibu wa kukabidhi madaraka kwa wananchi. Taarifa ya mapendekezo ya ujumbe huo ndiyo iliyowezesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha Azimio Na 435 ya mwaka 1978 ambayo hatimaye yalileta uhuru wa Namibia.

1990: Mark Bomani aliandaa katiba mpya ya Namibia baada ya kupata uhuru

1991: Mark Bomani aliombwa kuwa Jaji Mkuu wa Namibia lakini badala yake akaomba awe mshauri wa masuala ya Sheria na Katiba kwa miaka miwili tuu akiamini kwamba muda huo ungetosha kabisa kutoa mchango wake kwa wana-Namibia.

1992: Bomani aliteuliwa na Rais Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Wataalam wa Zanzibar na wa Tanzania Bara iliyoundwa kutoa mapendekezo juu ya namna ya kumchagua Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na mgawanyo wa madaraka kati yao na Bunge. Rais Mwinyi pia alimteua Mark Bomani kuwa Jaji.

1993: Mwenyekiti wa Kamati Maalum (Legal Task Force) iliyopewa jukumu la kukarabati sekta yote ya Sheria nchini, chini ya mradi wa Benki ya Dunia, Wahisani mbalimbali.

1993:1995: Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

1993: Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji

1995: Bomani ajitosa siasa kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwa mgombea Rais.

1995:
Baada Mwalimu Nyerere kuchaguliwa kuwa Mpatanishi wa mgogoro wa Burundi na Umoja wa Mataifa na OAU, Nyerere akamuomba Bomani kuwa msaidizi wake kazi aliyoifanya mpaka Mwalimu Nyerere alipofariki mwaka 1999. Baada ya Nelson Mandela kuchaguliwa kuwa mpatanishi mpya, Bomani akawa msaidizi wake na kwa pamoja wakaweza kufanikisha azma ya kupatanisha pande husika mnamo Agosti 2000.

2007:
Rais Kikwete alimteua Bomani kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya watu 12 kupitia upya sera ya madini.

2018:
Mwenyekiti wa CCM, John J.P. Magufuli alimteua kuwa mmoja wa wajumbe watano wa Bodi ya Kwanza ya Udhamini ya CCM.

Mark Bomani aliendelea na shughuli za uwakili kupitia kampuni yake ya Bomani & Company Advocates. Mark Bomani alikuwa mkurugenzi na muanzilishi wa kampuni ya Serengeti Breweries. Pia alikuwa mkurugenzi wa Bodi ya Benki ya NCBA.


Baadhi ya mada kuhusu Jaji Bomani
Jaji Bomani, Mkapa, mramba, Kigoda, Chenge. Wote hawa walisababisha serikali hasara ya mabillions tokana na mrahaba wa madini 3%. Leo hii Tanzania uchumi wake ungekuwa juu sana, tokana na tamaa zao za mali Kama alivyosema JPM kwamba hawakufanya hivyo bila kupata % ambayo iliingizwa kwenye maakaunti yao uko nje, wakati huo watanzania wanakuwa fukala, madini yanapelekwa nje Tena kwa escort ya ulinzi mkali. Kati ya hao aliye hai ni Chenge tu wengine wameshatangulia mbele ya haki. Uko waliko wanaona makosa waliyofanya kwa watanzania au binadamu wenzao. Lakini binadamu hajifunzi makosa ya watangulizi wao leo hii unaona watu wanafanya mambo ya ovyo kwa ajili ya familia zao. Hawajui hao waliotangulia walikuwa Kama wao. Tenda mema kwa binadamu mwenzako maana hujui siku Wala saa. Mali na utajili hutakwenda navyo mwishoni utawekewa nondo na zege hili usitoke humo na Wala harufu yako wasisikiye wanaopumua bado uko duniani. Baada ya miaka 20-50 hilo sanduku la mbao linaanza kuliwa na mchwa wakati wewe uko ndani kimeshabakia fuvu lako vingine vimeshaoza na kupukutika na kuwa unga. Tutende mema kwa Wana dunia.
 
MToronto
Kabisa. Huwezi jua wanamiliki majengo pale mjini kati na Upanga. Hata mwanae wa kike bibi Rhoda (Marehemu)alikuwa low profile sana.
Wake yule clement bomani rafiki yangu sana miaka nenda rudi

Ova
 
Back
Top Bottom