Mwanasheria Mkuu wa serikali aingilie kati, haiwezekani kila ardhi yenye hati, kesi yake ifunguliwe Mahakama Kuu, hatuna nauli kuja mjini

Mwanasheria Mkuu wa serikali aingilie kati, haiwezekani kila ardhi yenye hati, kesi yake ifunguliwe Mahakama Kuu, hatuna nauli kuja mjini

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nadhani mwanasheria Mkuu wa serikali ayaangalie mapungufu katika ofisi ya wakili Mkuu wa serikali. Kama mwendesha mashtaka wa serikali (Dpp)anaweza kuendesha mashtaka mpaka mahakama ya wilaya au ya mwanzo, na wana ofisi huko, kwa nini hawa wa Wakili Mkuu wa serikali sheria isiweke utaratibu kuishtaki serikali huko huko ngazi ya wilaya, walau katika ardhi yenye thamani ya wastani, huko Mahakama Kuu wabaki na makesi yao makubwa makubwa, yaani kweli hata Skwea mita 400 huko kijijini ndani iende kwa prezdensho apointii? Wao wa Wakili Mkuu iwe Mahakama Kuu kwa umaalum upi?

Yaani nimepambana nimepata hati miliki, ikiwa na shida nisafiri mamia ya kilometa na nikalale gesti, niamkie mahakamani? Si bora nisiwe na hati au bora nikasake unga wa miti na makopela ya kwa msisi nitwangane na mwenzangu? Kwanza yana bei rahisi kuliko kutafuta Wakili wa kuandaa kesi.

Kuna haja ya kubadili sheria, kesi za vijiji, hati, zianzie wilayani. Hao viongozi wa vijiji mtawaua na hizo gharama za kuja mijini

Hao majaji waliolemewa ndio mnawapa mzigo mkubwa wa kusikiliza malaki ya mashauri ya hati?
 
Tulielewana kuwa mama anaupiga mwingi
 
Back
Top Bottom