Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Watumishi acheni kuvujisha siri za Serikali, ni sawa na kujipiga risasi ya kwenye moyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Your browser is not able to display this video.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza S. Johari amesema kuwa ofisi yake ya Mwanasheria mkuu wa Serikali itawafuatilia watumishi wenye tabia za kutoa Siri za Serikali na wenye tabia za uongo

Mhe. Hamza ameyasema hayo Leo Agost 18,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza kwenye Baraza la wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria mkuu wa Serikali

Mhe. Hamza amesema kuwa hivi karibuni kumeibuka tabia za watumishi kutoa Siri za ofisi huku wakifahamu kufanya hivyo ni kinyume na Sheria na miongozo ya Nchi

Mhe. Hamza amesema kuwa watumishi hao wahakikishe hawatoi taarifa za Ofisi bila kibali kwani kufanya hivyo ni kujipiga Risasi wao wenyewe

Aidha, Hamza amesema kuwa wapo baadhi ya mawakili wa Serikali waongo hali inayopelekea kutia aibu kwenye Taaluma na Ofisi.
 
Siri za mikataba ya DP world, mikakati ya sheria za unyanyasaji na utekaji , list za wakwepa kodi wachangiaji wa CCM na kushidwa kwa kesi za nje ni bora zivujishwe kwa manufaa ya umma
 
Mtu hawezi kuvujisha siri nzuri inayotakia mema taifa letu.

Ukiona imevujishwa ni siri ovu inayolenga kuumiza mtu au taifa.
 
Siri za kuua watu? Zisivuje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…