Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aikataa Katiba

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar aikataa Katiba

Zanzibar kumekucha , Othman Makungu kaamua kuwaeleza ukweli Mbulula wa CCM ......
Mungu amesikia kilio chetu, nazidi kuomba " Eeee, Mungu muumba wa mbingu na nchi sikia kilio chetu bunge hili lililo tupa maadili na uwajibikaji na livunjike vunjike bila kuelwana, Mungu wewe ni wa maadili embu ona wametoa tunu za taifa sasa wameweka mambo ya siasa, bora uwaharibie usemi wasielewane."
 
Samweli sitta aache upuuzi wake….
Na wabunge wa cuf watakaokubali rasimu watengwe maisha yao woote
 
Ibara alizikataa 2,9,.....,70-75,128,129,158-159,160,161,242-251 & nyongeza 1(70)
 
Dah! Mambo mengine ni magumu sana kuyaelewa, huyu ndiye mshauri mkuu wa sheria wa rais na serikali ya znz. Nauliza tu kwa anaejua, kauli yake si ndiyo kauli ya serikali ya znz?

Hakika mkuu ila kwa sababu ya mgawanyiko wa wazanzibari ndani ya hilo bunge wala hawez kuheshimiwa kama katoa kauli ya serikali nyingi itakuwa vijembe na kejeli dhidi yake,mambo mengi yako desperate ndani ya serikali kwa ujumla!
 
Samuel Sitta ukafie mbali. Mwisho wako umekuwa mbaya kuliko mwanzo wako. Poor you!
 
Ndugu Safari_ni_Safari huyu mwanasheria mkuu na kura yake kwa mtazamo wangu ni kama kura ya Wazanzibari Wote.

Hapana mkuu kwenye bunge maalumu la katiba hawapigi kura kwa vyeo vyao bali wote ni wajumbe wa kawaida wa bunge hilo. Kwa hiyo kura yake ni yake binafsi kama yeye.
 
Dah! Mambo mengine ni magumu sana kuyaelewa, huyu ndiye mshauri mkuu wa sheria wa rais na serikali ya znz. Nauliza tu kwa anaejua, kauli yake si ndiyo kauli ya serikali ya znz?

Mkuu, rais akishachaguliwa na kabla ya kuunda serikali (baraza la mawaziri) lazima kwanza ateue mwanasheria mkuu ili washirikiane kuunda serikali. Kwa muktadha huo ulichosema ni sahihi.
 
Hii ni tetesi nimeipata kwamba ili akidi ipatikane,watu wenye nguo za kiraia walimfikisha na kuhakikisha ameingia, akidi inatafutwa! Natafuta taarifa zaidi,nina wasiwasi wajumbe wengine pia wanaweza kuletwa under the same style,mwenye uhakika zaidi afunguke au mwanasheria mwenyewe
 
Mwanasheria mkuu Zanzibar - MSIMAMO WAKE WA KUIGWA.Naamini ktk uhuru na haki ya kutoa maoni sio lazima kila jambo ukalikubali tuu kisa uko upande wa walio wengi,msimamo ni jambo la heri pale tuu ukiwa na msimamo wa haki na usawa kwa kila pande,ukweli daima utakuweka huru,na mwenyezi mungu atakurehemu kwa msimamo wako wa haki.Nampongeza sana Mh mwanasheria mkuu toka Zanzibar kwa msimamo wake.pamoja na vitisho vyote toka upande huu.
 
...fafanua kidogo,huku mwanakwerekwe tuko makini kusikiliza hayo majamaa yanayo taka kuburuzana...
 
Katiba upatikana kwa maridhiano pasipo na maridhiano hakuna katiba, haya maguvu yanayotumiwa na maCCM yatatuletea machafuko kama yale yaliyotokea nchini Kenya na wanatakiwa wajue sisi wananchi tunawajua vema wapambe, wanachama na wapenzi wa CCM lakini sisi hawatujui hivyo wakituingiza kwenye machafuko wajue wamekwisha kwani hata JWTZ na Polisi hawatakuwa upande wao NYAMBAFU!!!!!
 
Mijitu ya CCM bila aibu imeshupalia afukuzwee! afukuzwee! sasa ndugu zangu matafukuzaje mtu kisa katumia haki yake kidemokrasia kupiga kura ya hapana tena kwa wazi? kama wajumbe wote walitakiwa kuitikia ndioooooo! kama mazombi vile! kulikuwa na haja gani ya kuweka utaratibu wa kura?
 
Hapana mkuu kwenye bunge maalumu la katiba hawapigi kura kwa vyeo vyao bali wote ni wajumbe wa kawaida wa bunge hilo. Kwa hiyo kura yake ni yake binafsi kama yeye.

Upo sawa ndio maana hata yule alieomba mwongozo nimemshangaa sana
 
Back
Top Bottom