Mwanasheria pitia hapa

Mwanasheria pitia hapa

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
4,664
Reaction score
9,929
Naomba kujua hivi sheria inasemaje pale mtu anakuletea mkataba ambao anasema umeusign wewe ukiangalia mwandiko na sign vinafanana kabisa na wako pia kaattach na copy za ID original zako akidai wewe ndie ulisign lakini kiuhalisia ukusign wewe ni uhuni umefanyika tu kufanya uonekane ni wewe

Je ushahidi upi unaitajika kuomba ili kuthibitisha ni Mimi kweli nilisign si kama amefodge
 
Tuanze hapa.

hizo copy za id original zilikuwa certified?

Si unajua copy zinakuwaga certified kama ni copy ya original na kamishna wa viapo/wakili.

Sasa kama hazijawa certified tumia utetezi huo kuwa copy walizoleta jambo zinafanana na vitambulisho vyako hazijawa certified na kama kama zilikuwa certified aje kutoa ushahidi huyo aliyecertify copy hizo
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
kwahiyo unaweza kuwarudishia mpira kuwa wamefabricate documents kutokana hazijawa certified.

na pia kama kwenye hiyo mikataba kuna mashahidi waitwe waje watoe ushahidi mbele ya mahakama
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Police case then watatafuta watalaamu wa maandishi ku baini muhusika
 
Naomba kujua hivi sheria inasemaje pale mtu anakuletea mkataba ambao anasema umeusign wewe ukiangalia mwandiko na sign vinafanana kabisa na wako pia kaattach na copy za ID original zako akidai wewe ndie ulisign lakini kiuhalisia ukusign wewe ni uhuni umefanyika tu kufanya uonekane ni wewe

Je ushahidi upi unaitajika kuomba ili kuthibitisha ni Mimi kweli nilisign si kama amefodge
Vitu ambavo vinaweza kubatilisha mkataba mkuu kwa haraka haraka ni kama vifuatayo;

1) Misrepresentation - hapa ukiweza kuithibitishia mahakama kua pande moja haikua wazi/mkweli juu ya jambo la kimkataba. Either kwa kizembe au kwa makusudi. Kwa njia moja au nyingine.

2) Mistake - Pindi pande moja au zote hazikuelewa au lilifanya kosa/jambo fulani la kimkataba.

3) Duress - Mmoja alitumia nguvu kumlazimisha mwingine kuingia mkataba huo.

4) Undue Influence - Pande moja ilitumia vishawishi kumlaghai pande ya pili kuingia mkataba, kama vile kutumia ulevi, dawa za kuondoa akili na kadhalika.

5) Illegality - Uharamu wa mkataba, kua mkataba unalazimu pande moja kufanya jambo lisilo la kisheria.

Hayo maelekezo ni ya haraka haraka tu. Ni vyema ukipata ushauri wa mwanasheria unaemfahamu.

I stand to be corrected learned brothers and sisters..
 
Sawa
Tuanze hapa.

hizo copy za id original zilikuwa certified?

Si unajua copy zinakuwaga certified kama ni copy ya original na kamishna wa viapo/wakili.

Sasa kama hazijawa certified tumia utetezi huo kuwa copy walizoleta jambo zinafanana na vitambulisho vyako hazijawa certified na kama kama zilikuwa certified aje kutoa ushahidi huyo aliyecertify copy hizo
nimekupata mkuu
 
Vitu ambavo vinaweza kubatilisha mkataba mkuu kwa haraka haraka ni kama vifuatayo;

1) Misrepresentation - hapa ukiweza kuithibitishia mahakama kua pande moja haikua wazi/mkweli juu ya jambo la kimkataba. Either kwa kizembe au kwa makusudi. Kwa njia moja au nyingine.

2) Mistake - Pindi pande moja au zote hazikuelewa au lilifanya kosa/jambo fulani la kimkataba.

3) Duress - Mmoja alitumia nguvu kumlazimisha mwingine kuingia mkataba huo.

4) Undue Influence - Pande moja ilitumia vishawishi kumlaghai pande ya pili kuingia mkataba, kama vile kutumia ulevi, dawa za kuondoa akili na kadhalika.

5) Illegality - Uharamu wa mkataba, kua mkataba unalazimu pande moja kufanya jambo lisilo la kisheria.

Hayo maelekezo ni ya haraka haraka tu. Ni vyema ukipata ushauri wa mwanasheria unaemfahamu.

I stand to be corrected learned brothers and sisters..
hizi zote haziingii kabisa maana huo mkataba yeye hajausaini kabisa na wala hajui vitambulisho vimetoka wapi japokuwa ni copy original ya vitambulisho vyake.
 
Kama kuna sign yake wameifoji basi lazima hio MISREPRESENTATION inahusika, katika misrepresentation kuna swala linaitwa FRAUDULENT MISREPRESENTATION... kwamba wamedhamiria kulifanya hilo swala la kufoji sign bila idhini yake... pia kama atafanikiwa kuuvunja anaweza kuwaanzishia kesi ya jinai juu la hilo swala la kufoji sign/nyaraka
 
misrepresentation ni kama mtu akudanganye ana AB au kuna AB wakati ana XX au YY..

Huu mkataba yeye haujui kabisa wala hajawahi kukaa nao kuujadili its a total fabrication, sio sahihi kusema kuna misrepresentation kwenye kitu ambacho kwake hakipo.

Na sio sahihi kusema yeye auvunje huo mkataba maana hajawahi kuuingia , huwezi ukavunja mkataba ambao hujawahi kuingia na wala hauujui, issue ni kwamba hao walioleta mkataba wathibitishe kuwa waliingia kweli mkataba na mleta mada na itakapohitajika mleta mada atoe uthibitisho kuwa huo mkataba ni forged document.
 
Kama kuna sign yake wameifoji basi lazima hio MISREPRESENTATION inahusika, katika misrepresentation kuna swala linaitwa FRAUDULENT MISREPRESENTATION... kwamba wamedhamiria kulifanya hilo swala la kufoji sign bila idhini yake... pia kama atafanikiwa kuuvunja anaweza kuwaanzishia kesi ya jinai juu la hilo swala la kufoji sign/nyaraka
Yeye hana uwezo wa kuwaanzishia jinai, adai tu damages
 
Back
Top Bottom