figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salaam Wakuu
Kipindi cha Kampeni, kumekuwa na tabia ya Wanasiasa ya kubandika Mabango ya Kampeni kwenye Mitaa, Barabarani na hata kwenye kuta za nyimba za watu. Lakini Uchaguzi Ukiisha hawarudi kuondoa mabango yao ambayo yanageuka Uchafu Mitaani.
Tamisemi isisimamie kura tu na hesabu bali isimamie na mazingira kwa kuwapa muongozo Wagombea kuondoa Mabango baada ya Uchaguzi. Watoe muongozo kiasi kwamba kama mtu atakiukwa chama chake kipigwe faini.
Pia Watoe muongozo sehemu za kubandika hayo mabango ya Kampeni. Kuna chama kinaweka makaratasi ya Kampeni kadi Ofisi za Umma na Sehemu zinazotoa huduma za Umma. Pamoja kwamba Uchaguzi ni kitu Muhimu, pia Mazingira yetu ni muhimu zaidi. Tuyatunze yatutunze.
Wagombea wa vyama vya Siasa waonywe ili waache tabia ya kubandika Mabango kiholela. Pia Wasibandike kwenye eneo au nyumba ya mtu bila kuomba ruhusa kwani huwa yanachanwa na kutapakaa njiani.
Kama tunavyojua kubandika mabango ya kampeni, matangazo au mchoro wowote kwenye nyumba, majengo au vyombo vya usafiri vya watu binafsi au taasisi mbalimbali bila idhini ya wamiliki husika ni kosa na kubandika mabango ya kampeni, matangazo au mchoro wowote kwenye nyumba za ibada, taasisi za dini na majengo ya Serikali na taasisi zake ni kosa. Lakini watu wamekuwa wakifanya hivyo na hakuna hatua zinachukuliwa.
Pia soma: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Nyuzi za Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024