Mwanasiasa / Kiongozi mkubwa kutoa ' Tamko ' pasipo ' Ukomo ' wake ni Kiashirio cha Uweledi wake au Kupotoka Kwake?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Viongozi wengi wa Mataifa mengi ( Barani Afrika, Ulaya, Marekani na hadi Asia ) nimeona wakiweka Ukomo katika Matamko yao hasa juu ya hili Janga baya la CORONA ( COVID-19 ) ila nasikitika Viongozi wa Mataifa mengine wamekuwa wakitoa tu Matamko yao pasi na Kuwaeleza Wananchi ni lini kutakuwa na Ukomo.

Labda tu niwaambie hao Viongozi kwamba Kitu pekee wasichokijua sasa ni kwamba wameshawazidishia Mawazo na Machungu Wananchi wao kwani hao Wananchi Wao sasa wanawaza ni lini Janga hili la CORONA litamalizika ili Maisha yao magumu yaendelee lakini pia sasa wapo njia panda kujua kama Watoto wao wataendelea na Masomo au Likizo yao itakoma ( itaisha ) rasmi January 2023.

Nichukue nafasi hii adhimu kuwapongeza Marais na Viongozi mbalimbali wa nchi zingine zinazojielewa kama India, Marekani, Germany, Spain, Uganda, South Afrika, Rwanda, Kenya, Iran, Uingereza, Ghana, Sweden na Ufaransa ambao Wao licha ya kwamba CORONA inawatesa na wengine wana ' both Partial and Total Lock down / Curfew ' lakini kila wakijitokeza Kuzungumza na Wananchi wao hawasahau kusema ' Ukomo ' wa tarehe juu ya ' Matamko ' yao.

Mwenyezi Mungu atusaidie.
 
Nakumbuka wakati nipo form 3 kulitokea fujo shule na shule ikafungwa muda usiojulikana nilikaa nikajiuliza nikasema siendi nyumbani liwalo na liwe

Nikazama mtaani Tabora nikaanza kupiga vibarua kipindi icho sina hata phone nikapiga vibarua mpaka masomo yakalejea bila home mshua kujua chochote

Wanaume tunapitia mengi sana maani hata sasa kuna vijana wamejizamia tu kutafuta pesa wanajua kabisa kwenda home bila ratiba ni michosho hasa wenye washua wakorofi wakorofi

Ningeenda home nikawaambia shule imefungwa kisa fujo pangechimbika

Halafu muda usiojulikana halafu ukizingatia mshua alikuwa ni wale wa mabaka mabaka.
 
Yeye ni Mungu hadi ajue tatizo linaisha lini. Pili nadhani wananchi wa hizo nchi hawana tabia za kijinga kama za watanzania.
 
POINT ni zile zile
Lack of enough capital
Financial instability
Lack of funds
Lack of international cooperation
Lack of national and International Collaborations
Poor government support (policies and taxes)
Poor infrastructure (housing, communications and transports)
Lack of social education
Poor and cheap labour skills
Natural calamities and disaster (floods)
Epidermic Disease (like Corona)
Overpopulation
High dependency ratio
Language barrier
Hostility communities
Unaweza kuongeza na zako pia
 
Nakumbuka wakati nipo form 3 kulitokea fujo shule na shule ikafungwa muda usiojulikana nilikaa nikajiuliza nikasema siendi nyumbani liwalo na liwe

Nikazama mtaani Tabora nikaanza kupiga vibarua kipindi icho sina hata phone nikapiga vibarua mpaka masomo yakalejea bila home mshua kujua chochote

Wanaume tunapitia mengi sana maani hata sasa kuna vijana wamejizamia tu kutafuta pesa wanajua kabisa kwenda home bila ratiba ni michosho hasa wenye washua wakorofi wakorofi

Ningeenda home nikawaambia shule imefungwa kisa fujo pangechimbika

Halafu muda usiojulikana halafu ukizingatia mshua alikuwa ni wale wa mabaka mabaka.

Ukitaka kuwa mfuasi real wa CDM, ongeza Elimu yako.
 
Ndio uwezo ulipoishia kwa sasa! Amesema kwa niaba ya serikali.
State organs zimeshindwa kuunda mikakati mahususi iinayotekelezeka ikionyesha 'pumzi' ya kupambana, na taswira ya pambano ilivyo/itakavyokuwa.
Ni sawa kusema, ingekuwa ni mpira (kwa mfano tu), hakuna cha kuwapa hamasa mashabiki.
Naonaga wadau wanakabidhi mamilioni, ila harakati za kweli - kufa ama kupona sizioni wala sizikii.
NAHISI tunapambana kiboya sana!
NDIO ISHARA HALISI YA UMASKINI!
Kama huko dunia ya kwanza wanaweka mipango, wanakomaa wee, wanaipangua na kupanga tena, ... Je huku ulimwengu wa tatu?
 
Viongozi wengi wa Mataifa mengi ( Barani Afrika, Ulaya, Marekani na hadi Asia ) nimeona wakiweka Ukomo katika Matamko yao hasa juu ya hili Janga baya la CORONA ( COVID-19 ) ila nasikitika Viongozi wa Mataifa mengine wamekuwa wakitoa tu Matamko yao pasi na Kuwaeleza Wananchi ni lini kutakuwa na Ukomo.

Labda tu niwaambie hao Viongozi kwamba Kitu pekee wasichokijua sasa ni kwamba wameshawazidishia Mawazo na Machungu Wananchi wao kwani hao Wananchi Wao sasa wanawaza ni lini Janga hili la CORONA litamalizika ili Maisha yao magumu yaendelee lakini pia sasa wapo njia panda kujua kama Watoto wao wataendelea na Masomo au Likizo yao itakoma ( itaisha ) rasmi January 2023.

Nichukue nafasi hii adhimu kuwapongeza Marais na Viongozi mbalimbali wa nchi zingine zinazojielewa kama India, Marekani, Germany, Spain, Uganda, South Afrika, Rwanda, Kenya, Iran, Uingereza, Ghana, Sweden na Ufaransa ambao Wao licha ya kwamba CORONA inawatesa na wengine wana ' both Partial and Total Lock down / Curfew ' lakini kila wakijitokeza Kuzungumza na Wananchi wao hawasahau kusema ' Ukomo ' wa tarehe juu ya ' Matamko ' yao.

Mwenyezi Mungu atusaidie.
Wewe jamaa unakuaga na akili kubwa sana. Laiti watu hata robo wangekuwa na akili kubwa kama ya kwako na wakaweza kukuelewa na kutenda kama unavyosema ingekuwa ni asali na maziwa tu kila siku, uandishi wako nakubali sana
 
Corona ni ugonjwa mkubwa kuliko hizi siasa zetu za lawama zinavyotudanganya. Ni ugonjwa wenye madhara makubwa kimwili, kijamii na kiuchumi.

Donald Trump anauficha udhaifu wake kwa kuinyima WHO pesa kama kisingizio cha uongozi wake kutokuwa umejiandaa kukabiliana na ukubwa wa pandemic.
 
With what measures can u have the guts to mention deadline?
 
Nakumbuka wakati nipo form 3 kulitokea fujo shule na shule ikafungwa muda usiojulikana nilikaa nikajiuliza nikasema siendi nyumbani liwalo na liwe

Nikazama mtaani Tabora nikaanza kupiga vibarua kipindi icho sina hata phone nikapiga vibarua mpaka masomo yakalejea bila home mshua kujua chochote

Wanaume tunapitia mengi sana maani hata sasa kuna vijana wamejizamia tu kutafuta pesa wanajua kabisa kwenda home bila ratiba ni michosho hasa wenye washua wakorofi wakorofi

Ningeenda home nikawaambia shule imefungwa kisa fujo pangechimbika

Halafu muda usiojulikana halafu ukizingatia mshua alikuwa ni wale wa mabaka mabaka.

Utakuwa umesoma kwa WANAUME-MILAMBO SS
 
Mbona huu mfano wako ni mbingu na ardhi?

Nyie mlifukuzwa sababu ya fujo, PM kafunga shule nchi nzima sababu ya ugonjwa hali ikitulia atakuja tena kutangaza siku ya kufungua shule na vyuo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe jamaa unakuaga na akili kubwa sana. Laiti watu hata robo wangekuwa na akili kubwa kama ya kwako na wakaweza kukuelewa na kutenda kama unavyosema ingekuwa ni asali na maziwa tu kila siku, uandishi wako nakubali sana

Asante sana Mkuu na ashukuriwe mno Mwenyezi Mungu kwa Neema yake hiyo uliyoiona ndani yangu. Tupo pamoja pia Mkuu.
 
Kwahiyo unasema Rwanda kiongozi wao ana akili sana? Mimi nadhani bado akujawa na madhala makubwa apo kwenu ila ningekua mimi ndiyo mkuu wenu kusema kweli ningewazidi wote hao ata Nicaragua wangejifunza kwangu.
 
Back
Top Bottom