MwanaSimba yeyote aniambie sababu zozote za maana za kumtimua Uchebe

MwanaSimba yeyote aniambie sababu zozote za maana za kumtimua Uchebe

His Simba? When and who gave him that tittle of being Simba owner? Tatizo wazee km kina kilomoni wanajifanyaga wanapiga kelele mianya ya kupiga pesa ikizibwa but wakiwa wanaambulia chochote kitu huwezi kusikia milele miaka yote aliyokaa Simba kwanini alishindwa kutafuta muwekezaji ambaye angeweza kuendana na terms & conditions alizokuwa anazitaka?
Mwanachama yeyte wa Simba , Simba ni yake.
 
Uchebe naye alianza kuyumba na hata angekuwepo hali ingekuwa kama hii tu.

1.Alikuwa ameanza kuishiwa mbinu, ndio maana Simba ilianza kushinda kwa bahati nasibu. Graph ya ushindi wa Simba ilikuwa na mwendo wa diminishing progression.

2.Mnatumia Simba kufika robo fainali CCL kama credit kwake, ila hamjui kuna mbinu za nyuma ya pazia zitumike kuifikisha pale. Angalia mechi za away alivyokuwa anafanya utumbo, timu ikiwa home ground watu walikuwa wanaingia mzigoni kumsaidia, yet alianza kusaidiwa anaanza kulalama anaingiliwa majukumu.

3.Timu ilianza kuwa na nidhamu mbovu chini yake.

4.Kwamba yeye alikuwa hafungwi kwenye ligi? Hamjui kuna point 5 tumepoteza chini ya Aussems kwenye TPL?

5.Eti kwanini alifukuzwa ilhali Simba inaongoza ligi? Jibu la swali hili rejea hapo no.1. Na hii ndo sababu inayofanya Barcelona nao wamtimue kocha wao Ernesto Velverde. Ilifika kipindi tulianza kukosa imani kama Aussems angetuvusha, sawa na Barcelona ambavyo wamekosa imani na Ernesto pamoja na timu hiyo bado kuwa kwenye msimamo mzuri wa La Liga. Tatizo lao wote ni moja; kadri ligi inavyosonga mbele timu zinaanza kushinda kwa bahati nasibu at a diminishing rate.
 
Kichwa cha habari chajieleza.

Kiwango cha Simba wakati wa Uchebe hakifanani kabisa na Simba hii chini ya kocha huyu mpya mwenye CV ya kusononesha.

Simba ya Uchebe haikuwahi kuzidiwa ball possession na vitimu vya nchi hii. Leo Mtibwa wamemiliki mpira kwa 51% huku Simba wakiwa na 49%, ni uchafu gani huu jamani?

Kwanini Uchebe aliondolewa bila sababu zenye mashiko?
Jibu umelipata Kiongozi. Ubabaishaji uliokithiri
 
Uchebe naye alianza kuyumba na hata angekuwepo hali ingekuwa kama hii tu.

1.Alikuwa ameanza kuishiwa mbinu, ndio maana Simba ilianza kushinda kwa bahati nasibu. Graph ya ushindi wa Simba ilikuwa na mwendo wa diminishing progression.

2.Mnatumia Simba kufika robo fainali CCL kama credit kwake, ila hamjui kuna mbinu za nyuma ya pazia zitumike kuifikisha pale. Angalia mechi za away alivyokuwa anafanya utumbo, timu ikiwa home ground watu walikuwa wanaingia mzigoni kumsaidia, yet alianza kusaidiwa anaanza kulalama anaingiliwa majukumu.

3.Timu ilianza kuwa na nidhamu mbovu chini yake.

4.Kwamba yeye alikuwa hafungwi kwenye ligi? Hamjui kuna point 5 tumepoteza chini ya Aussems kwenye TPL?

5.Eti kwanini alifukuzwa ilhali Simba inaongoza ligi? Jibu la swali hili rejea hapo no.1. Na hii ndo sababu inayofanya Barcelona nao wamtimue kocha wao Ernesto Velverde. Ilifika kipindi tulianza kukosa imani kama Aussems angetuvusha, sawa na Barcelona ambavyo wamekosa imani na Ernesto pamoja na timu hiyo bado kuwa kwenye msimamo mzuri wa La Liga. Tatizo lao wote ni moja; kadri ligi inavyosonga mbele timu zinaanza kushinda kwa bahati nasibu at a diminishing rate.
unastahili kupata balimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo si kuondoka Uchebe kwani kila mtu ataondoka Simba siku yake ikifika hata Mo ataondoka lakini unamleta nani wa kuziba pengo lake? Uchebe falsafa yake ni kushambulia kwa kwenda mbele akiwa na washambuliaji wawili kwa hiyo Simba iilikuwa inapiga kambi kwenye goli la timu pinzani muda wote wa mchezo. Huyu wa sasa hivi bado sijaelewa hasa falsafa yake ni ipi kwani mara nyingi naona anatumia mshambuliaji mmoja.

Kwa mfumo anaoutumia kocha mpya na msaidizi wake Matola wa mshambuliaji mmoja badala ya wawili wakati Simba ndio timu yenye viungo bora kabisa Tanzania natabiri hawa makocha pamoja na yule wa makipa hawana miezi miwili mbele watakuwa wameshatimuliwa.

Una Kagere na Boko wote wapo fiti halafu unampanga mmoja mwingine unamuweka benchi hapo ndio shida inapoanzia akishafichwa ng'ado kwa ng'ado (mtu na mtu) basi kwishney mashambulizi yaanahamia kwenu mnafungwa goli moja mpira umeisha halafu bado mnashangaa Mtibwa mwenye usajili wa milioni moja kachukuaje kombe mbele ya timu yenye usajili wa mabilioni.

Najua mzungu hakuwepo msimu uliopita lakini Matola alikuwa haoni ule utatu wa Kagere, Okwi na Boko ulivyokuwa unafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu? Kwa nini sasa Boko na Kagere wasianze pamoja halafu wakaongezewa mtu mmoja mbadala wa Okwi?

Na kwa mechi ya jana na mtibwa walaumiwe makocha kwa upangaji mbovu wa timu ukizingatia ilikuwa fainali. Walishindwaje kupanga wanaume 11 katikia kundi la wanaume na wavulana lenye watu zaidi ya 25?
 
tatizo la mashabiki na wanachama wengi wa simba walikuwa hawamsikilizi mzee Kilomoni wakamwelewa leo hii Mo anafanya maamuzi yake wanaanza kuhoji wakati nguvu ya kuhoji walishamkabidhi sasa hivi wakubali tu wawe washabiki kama wanavyoshabikia timu za ulaya
 
Marefarii bado kichomi kabisa, goli la fraga ni halali kabisa, jamaa alikuwa onside ila kutokana na presha za waamuzi kwenye mechi za simba tumenyimwa goli halali kabisa.
 
Marefarii bado kichomi kabisa, goli la fraga ni halali kabisa, jamaa alikuwa onside ila kutokana na presha za waamuzi kwenye mechi za simba tumenyimwa goli halali kabisa.
!!!
Screenshot_20200207-203306.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom