Mwanaspoti: Simba kupata pointi za mezani kwa Merrikh

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
sudan pic

SIMBA huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh kutokana na timu hiyo ya Sudan kudaiwa kuwatumia wachezaji wawili ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina yao uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliopita ambao uliisha kwa sare tasa.

Taarifa za uhakika ambazo uongozi wa Simba umedai kuzinasa kutoka Sudan kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, zimeonesha kuwa wachezaji hao Ramadan Agab na mwingine ambaye jina lake wanalisaka, walicheza mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA)

Ushahidi wa barua ambao Simba wameupata na kuionysha Mwanaspoti nakala, unaonyesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti, adhabu ambayo inaishia katikati ya Aprili.

"Hii ni nakala ya uamuzi. Kimsingi wachezaji hao wawili walisaini mikataba miwili tofauti na Al Merrikh na Al Hilal na wamefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita.

Barua hii ni ya Katibu Mkuu wa Al Merrikh ambayo walimpa kocha kwamba anaweza kuwatumia wachezaji wawili waliofungiwa. Wachezaji hao hawakucheza mechi yoyote ya Al Merrikh hadi sasa. Wamefungiwa kucheza hadi katikati ya Aprili. Wamefanya uamuzi wao wenyewe," alisema mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Ikiwa itabainika ni kweli Al Merrikh waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili kucheza, itaondolewa mashindanoni.

My Take
Nimefuatilia vyanzo mbalimbali nje ya nchi hapo kuna wachezaji wawili Mohamed Al-Rashed and Ramadan Agab. Mo Dewji na CEO Barbara fanyeni chap tujipigie point 3 na goli 2.

Screenshot_20210308-160628_Chrome.jpg
20210308_220823117215.jpg
 
sudan pic

SIMBA huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh kutokana na timu hiyo ya Sudan kudaiwa kuwatumia wachezaji wawili ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina yao uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliopita ambao uliisha kwa sare tasa.

Taarifa za uhakika ambazo uongozi wa Simba umedai kuzinasa kutoka Sudan kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, zimeonesha kuwa wachezaji hao Ramadan Agab na mwingine ambaye jina lake wanalisaka, walicheza mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA)

Ushahidi wa barua ambao Simba wameupata na kuionysha Mwanaspoti nakala, unaonyesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti, adhabu ambayo inaishia katikati ya Aprili
"Hii ni nakala ya uamuzi. Kimsingi wachezaji hao wawili walisaini mikataba miwili tofauti na Al Merrikh na Al Hilal na wamefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita.

Barua hii ni ya Katibu Mkuu wa Al Merrikh ambayo walimpa kocha kwamba anaweza kuwatumia wachezaji wawili waliofungiwa. Wachezaji hao hawakucheza mechi yoyote ya Al Merrikh hadi sasa. Wamefungiwa kucheza hadi katikati ya Aprili. Wamefanya uamuzi wao wenyewe," alisema mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Ikiwa itabainika ni kweli Al Merrikh waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili kucheza, itaondolewa mashindanoni.

My Take
Nimefuatilia vyanzo mbalimbali nje ya nchi hapo kuna wachezaji wawili Mohamed Al-Rashed and Ramadan Agab. Mo Dewji na CEO Barbara fanyeni chap tujipigie point 3 na goli 2.

View attachment 1720214
Eee mnayasahau ya Morrisson?
 
Sidhani kama kwa hadhi yako unastahili hoja butu kama hii, acha ikitokea itokee yenyewe.
 
Back
Top Bottom