Mwanaspoti: Simba kupata pointi za mezani kwa Merrikh

sudan pic

SIMBA huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh kutokana na timu hiyo ya Sudan kudaiwa kuwatumia wachezaji wawili ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina yao uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliopita ambao uliisha kwa sare tasa.

Taarifa za uhakika ambazo uongozi wa Simba umedai kuzinasa kutoka Sudan kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, zimeonesha kuwa wachezaji hao Ramadan Agab na mwingine ambaye jina lake wanalisaka, walicheza mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA)

Ushahidi wa barua ambao Simba wameupata na kuionysha Mwanaspoti nakala, unaonyesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti, adhabu ambayo inaishia katikati ya Aprili.

"Hii ni nakala ya uamuzi. Kimsingi wachezaji hao wawili walisaini mikataba miwili tofauti na Al Merrikh na Al Hilal na wamefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita.

Barua hii ni ya Katibu Mkuu wa Al Merrikh ambayo walimpa kocha kwamba anaweza kuwatumia wachezaji wawili waliofungiwa. Wachezaji hao hawakucheza mechi yoyote ya Al Merrikh hadi sasa. Wamefungiwa kucheza hadi katikati ya Aprili. Wamefanya uamuzi wao wenyewe," alisema mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Ikiwa itabainika ni kweli Al Merrikh waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili kucheza, itaondolewa mashindanoni.

My Take
Nimefuatilia vyanzo mbalimbali nje ya nchi hapo kuna wachezaji wawili Mohamed Al-Rashed and Ramadan Agab. Mo Dewji na CEO Barbara fanyeni chap tujipigie point 3 na goli 2.

View attachment 1720214
hiyo barua mstari wa pili ndio wamejichanganya, soma mwenyewe uone
 
Dah, barua inajieleza wazi kabisa! kama sio forged, simba anakula point tatu muhimu.
 
Nyau fc chezeni mpira mnataka vya mezani mtakuja kupakatwa live
 
Ikibainika ni kweli wataondolewa kabisa kwenye mashindano, na watakao umia ni Ahly na VITA
Hawataondolewa kabisa!! Hao wachezaji wanaolalamikiwa hawakucheza mechi za Vita na Al Ahly. Simba atapewa point 3. Mechi zijazo hawatawatumia hao wachezaji.
 
U mbumbumbu ni kipaji.kitu ambacho awafahamu mchezaji aliye fangiwa na FA husika anaweza funguliwa na FA husika dk yoyote tena kwa e- mail au fax tu wao FA husika ndio wanao amua. Nikama Yanga walivyo porwaa Morrison ni maamuzi ya FA husika kwa kutumia Nguvu na mamlaka. FA husika ilisha waidhinisha ao wachezaji kucheza El mereikh katika michuanomya CAF.
 
sudan pic

SIMBA huenda ikapata ushindi wa mezani dhidi ya Al Merrikh kutokana na timu hiyo ya Sudan kudaiwa kuwatumia wachezaji wawili ambao hawakupaswa kucheza katika mchezo baina yao uliochezwa jijini Khartoum, Jumamosi iliopita ambao uliisha kwa sare tasa.

Taarifa za uhakika ambazo uongozi wa Simba umedai kuzinasa kutoka Sudan kwa ushahidi wa nyaraka mbalimbali, zimeonesha kuwa wachezaji hao Ramadan Agab na mwingine ambaye jina lake wanalisaka, walicheza mechi hiyo huku wakiwa wanatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita waliyopewa na Chama cha Soka Sudan (SFA)

Ushahidi wa barua ambao Simba wameupata na kuionysha Mwanaspoti nakala, unaonyesha kuwa SFA iliwafungia wachezaji hao kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mikataba katika timu mbili tofauti, adhabu ambayo inaishia katikati ya Aprili.

"Hii ni nakala ya uamuzi. Kimsingi wachezaji hao wawili walisaini mikataba miwili tofauti na Al Merrikh na Al Hilal na wamefungiwa kucheza kwa muda wa miezi sita.

Barua hii ni ya Katibu Mkuu wa Al Merrikh ambayo walimpa kocha kwamba anaweza kuwatumia wachezaji wawili waliofungiwa. Wachezaji hao hawakucheza mechi yoyote ya Al Merrikh hadi sasa. Wamefungiwa kucheza hadi katikati ya Aprili. Wamefanya uamuzi wao wenyewe," alisema mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez.

Ikiwa itabainika ni kweli Al Merrikh waliwachezesha wachezaji ambao hawakustahili kucheza, itaondolewa mashindanoni.

My Take
Nimefuatilia vyanzo mbalimbali nje ya nchi hapo kuna wachezaji wawili Mohamed Al-Rashed and Ramadan Agab. Mo Dewji na CEO Barbara fanyeni chap tujipigie point 3 na goli 2.

View attachment 1720214View attachment 1720457
Hawatapata,wale jamaa wanakibali cha caf kuwachezesha hao wachezaji
 
Back
Top Bottom