Mwanaume akikupenda na kukuhitaji katika maisha yake hakosi namna yakukupata

Mwanaume akikupenda na kukuhitaji katika maisha yake hakosi namna yakukupata

Na hutoweza kuelewa.

Zingatia namna ya uwasilishaji wa fasihi simulizi na fasihi andishi utaelewa.matumizi ya lugha nyepesi na lugha mkanganyiko kama hii.

😜😜lengo si usumbufu..bali kupima matumizi ya ubongo namna ya kung’amua vitu vigumu 🤪🤪
Haya bana mpe Hi! Jamaa
 
Hello...hello...hello...😍

Hamjambo jamani huku ndani? Nina imani nyote mnaendelea vyema sana. 🤸‍♀️🤸‍♀️

Sasa basi, sijui huu ni ushuhuda, elimu, au uvumilivu. Hebu nyie someni halafu muone inakaa kwenye nini. 😁

Nisiwapotezee muda jamani, mambo ni mengi.

Sijui nilibahatika au ni kweli kuwa kuna wanaume wako hivi? Sijui lakini yote kwa yote, wacha nililete mezani.

Ninaamini mwanaume akikupenda na kukuhitaji katika maisha yake, huwa hakosi namna ya kuweza kukupata (hapa nieleweke sio kwa kulazimisha kumtoa mwanamke kwa mwanaume mwenzako. Hapa ni pindi ukijua hana mtu. Ukatumia pesa kumtoa mwanamke kwa mwanaume... 😁😁 My friend, kuna siku atapatikana mwenye pesa zaidi nawe utatolewa. 😃😃) Mapenzi ya kiwaki kishenzi.

Basi bhana, jamaa aliniimbisha songi muda mrefu kiaina. Sikuwa nikielewa, akili ilikuwa inawaza wali maharage tu. 🤣🤣 (Kiukweli sikumtilia maanani kabisa mtongozo wake.) Siku zikaendaaaaa. 😁😁 Siku moja akaniomba tufanye walking, sikuvunga siku hiyo.

Nikapiga kipensi, t-shirt, raba, na kofia, haooo tukaanza walking mdogo mdogo. 😁😁 Akaniambia "u look gud🥰🥰," kichwa kikajaa. 😁 Tukaendelea kubadilishana story za hapa na pale (tuko kwenye mazingira ya kuonana kila mara na huyu mwamba alikuwa ni mshkaji kwa muda kama wa miaka mitatu, so hiyo walking ilikuwa ni ya kawaida kabsa).

Kati ya story nyingi za kawaida tulizopiga siku hiyo ni pamoja na "mara ya mwisho kucheki afya ni lini?" Akaniuliza, nikamjibu. Na mimi nikamuuliza, "na wewe lini ilikuwa mara ya mwisho?" Akanijibu. 😁😁

Akaendelea... "Kwahiyo nikisema tupime afya sasa hivi uko tayari?" Nikamjibu ndio. 😁😁 Kichwa yake mbaya sana huyu mwamba, kwahiyo alifikiri nitaogopa. 🤣🤣

Akaniuliza ratiba yangu ya wiki mbili zijazo, nikamjibu. Tukaishia hapo kwenye mazungumzo, tukaendelea na walking.

Siku moja ndani ya zile wiki mbili, akaniuliza siku fulani utakuwa wapi? Nikamjibu nitakwenda sehemu fulani (anaijua) kwa muda wa siku tatu, akasema sawa, kila mtu akaendelea na mambo yake. 😊

Siku ya pili kati ya zile siku tatu, akaniambia yuko hiyo sehemu niliyopo, amekuja kwa ajili yangu (hapo tayari akili yangu imeshaacha kuwaza wali ndondo. 😊😊) Ninamuangalia mwana kwa jicho la tofauti kabisa.

Nimejaribu kufupisha kidogo jamani pamoja na kuruka ruka baadhi ya vitu, lakini historia ikabadilika.

Mshkaji bhana, baada ya kubadilisha uhusiano wetu wa zamani na kuwa mpya, akanilia bati. 😁😁😁 Nakuja kustuka, mbona kama nimeliwa bati chakorii mimi. 😁😁 Woi, nikavunga kiaina, lakini dizaini kama nilimuelewa mwana.

Siku hiyo sina hili wala lile, simu ikaita, "Chakorii uko wapi?" Nikamjibu, "Niko sehemu fulani." Akasema, "Tukutane sehemu fulani, mie sawa." Tukakutana, stori mbili tatu, akaanza, "Chakorii, sina uwezo wa kukulipa kuwa na wewe kwenye mahusiano, lakini kuna kitu naweza fanya juu yako. Mimi ehee..." 😊

"Kuna biashara ninaifanya, naomba baadhi ya wateja wangu nikupatie wewe uwe unaingiza faida ya 350,000 kila mwezi au zaidi. Hiki ndicho ninachoweza kukifanya kwako," akasema. Nilimshukuru sana aise. 🙏 Ngoja nifupishe.

Huyu masta ninamuombea maisha marefu duniani, na Mungu azidi kumbariki kila inapoitwa leo.

Japo kwa kuruka ruka, hatimaye nimemaliza kuandika. 💃💃

🤸‍♀️🤸‍♀️🤸‍♀️
Yaani sijaelewa kabisa. Au ni yule msukuma wako?
 
Huu Uzi kumaanisha mtu hakumokosolewa yaani Uzi mrefu ivo afu mtu hajapikwa traaaako,,,,kama utarudi kumalizia SAWA ila nje nahapo sio sawa
 
Huu Uzi kumaanisha mtu hakumokosolewa yaani Uzi mrefu ivo afu mtu hajapikwa traaaako,,,,kama utarudi kumalizia SAWA ila nje nahapo sio sawa
 
Na Kwa aina hii ya kutokusoma kitu na kukielewa…ndio maana mnasaini mikataba mibovu kupindukia mnakuja kustuka Uko mikono mitupu.

Penda kusoma kitu,tafakari,tafuta maana zaidi ya moja,,rejea tena swala husika,soma tena…sasa chukua kati ya zile maana mbili ulizozipata..anangalia ni maana gani inafiti kwenye swala husika.

Mkurupuko si mzuri.siku kwenye huu uzi….hapana.utulivu ni muhimu kwenye kila kitu😁😁itakusaidia
Sawa ila wewe ni Dume sio Jike,

Jike hawezi kuandika hivo, wachache tulosomea Cuba tulifundishwa kujua jinsia ya mtu kupitia maandishi yake, analysis inaonesha wewe ni Dume unaletavtu story hapa za kufikirika
 
Hakika inahitaji watu wachache sana kuelewa.na wewe ni mmojawapo aise😘
Nimeanza kusoma alama za picha mdogo sana kama miaka Tisa,mshua wangu alikuwa anarudi na gazeti halafu ananipa katuni ya Mzee Kingo nimsimulie,basi mara napatia mara nakosea,baadae nikawa fundi😁
 
Huu Uzi kumaanisha mtu hakumokosolewa yaani Uzi mrefu ivo afu mtu hajapikwa traaaako,,,,kama utarudi kumalizia SAWA ila nje nahapo sio sawa
Zungusha ubongo kidogo mkuu.acha kujilemaza
 
Sawa ila wewe ni Dume sio Jike,

Jike hawezi kuandika hivo, wachache tulosomea Cuba tulifundishwa kujua jinsia ya mtu kupitia maandishi yake, analysis inaonesha wewe ni Dume unaletavtu story hapa za kufikirika
Ukiona nafaa kuwa mwanaume fresh tu.
Ukiona nafaa kuwa mwanamke shegaa tu.

Usiangalie miandiko utapote chifu
 
mwamba yuko very strategic sana... nimemuelewa!
 
Sio maokoto tu…hapana!ni maokoto yenye faida.

Soma Kwa umakini HA

habari ya siku dear
ndio hayo hayo mwenyewe huwa sikati tamaa nikidhamiria haijalishi nitasubiri kwa muda gani,

salama za masiku uko salama mama?
 
Back
Top Bottom