Mwanaume akutwa amefariki Mto Kijenge Arusha, mwili wake ukiwa umeharibika sana

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mtu mmoja wa jinsia ya kiume amekutwa amefariki dunia katika eneo la Mto Kijenge, mtaa wa Block J, kata ya Ngutoto, jijini Arusha.

Kwa mujibu wa mashuhuda, walipokuwa wakipita pembezoni mwa bonde hilo waliona kwa mbali mwili wa mwanaume huyo, ndipo wakatoa taarifa kwa viongozi wa eneo. Baadaye Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji walifika eneo la tukio na kuanza operesheni ya kuutoa mwili.

Mwili huo ulitolewa kwa kutumia kamba kutokana na bonde hilo kuwa na kina kinachokadiriwa kuzidi futi 200, hali iliyofanya zoezi la uokoaji kuwa gumu.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…