kikuku ndio nini? samahani sijaelewa.
however, hapa duniani hatuishi kwaajili yetu sisi wenyewe tu, maadamu upo kwenye jamii ya watu wanaoamini au waliozoea kitu fulani, au desturi fulani, hauwezi kuleta democracia ya ulaya kusema mtu yuko huru kuvaa, kuishi au kufanya chochote kile ambacho moyo wake unampenda, kwasababu haishi kisiwani, anaishi kwenye jumuiya ya watu hivyo lazima KILA MTU AHAKIKISHE ANAENDANA NA LIFE STYLE YA WATU WA ENEO LILE. unajua, kwangu mimi ninayeamini Biblia, hata kama kitu kwako ni kizuri kama umekifanya kwa mtu ambaye kwake anaona si kizuri na hauja mwelekeza akakubaliana nacho, ukikitenda icho kitu akakwazika kiasi cha kutomwamini Mungu kwa namna yoyote ile, kumkufuru Mungu au kwenda vibaya kwa jambo lolote lile kwasababu tu ya vile wewe ulivyofanya/behave etc, unakuwa umetenda dhambi pamoja na kwamba kitu hicho per se si dhambi, ina kinaweza kuwa converted kuwa dhambi kulingana na matumizi, mazingira etc.
kwahiyo, kama anavaa shanga na watu hawataki kuziona hapa mjini, basi aziweke kwenye begi hadi kipindi atakapotembelea kijijini kwake ambako kuna jumuiya yao tu ndo atavaa, kwa wanawake wa pande za Asia wengine huwa wanavaa shanga kwenye mguu na si kitu kibaya kwao, kama wakija hapa kwetu hawatakiwi kuvaa, wakivaa tukakwazika ni dhambi iliyokuwa converted kutoka kwenye kitu cha kawaida to a sin. kwa wazungu, etc, wanaovaa suluari wanawake, kama wakija kwenye kanisa ambalo mimi nasali au wewe unasali ambalo hawaamini kuvaa suluali, usivae, ukivaa ukawakwaza ni dhambi..OLE WAKE YEYE AMKWAZAYE HATA MMOJA TU WA WADOGO HAWA, ITAKUWA NI HERI KWAKE KAMA ANGEFUNGIWA SHINGONI MWAKE JIWE LA KUSAGIA AKATUPWE BAHARINI. mfano, ulaya na nchi zingine ambazo zina baridi, watu wote wanavaa suluari wanawake kwa wanaume, si rahisi kuona mtu amevaa lubega, ukivaa lubega unaweza kukwaza watu fulani pia, kwaiyo kila mtu anatakiwa ku switch to a particular community according to their ways of life anayoikuta pale.
kwa wanaume kuvaa heleni, kutoga na kutoboa masikio midomo pua na ulimi etc, wanaume kuvaa mavazi na kubehave kama wanawake, ni kitu ambacho hakikubaliki hapa Tanzania, hivyo mtu anayefanya hivyo anakwaza wengi, na hana cha kujitetea kusema kuwa, AAAH, MBONA NI MAISHA YANGU, MBONA SIOMBI HELA YA KULA TOKA KWA MTU, MBONA SIMDHURU MTU, MBONA MBONA...., ndo wanavyojitetea wengi wanaosuka nywele, wanaotoga masikio na midomo etc. they are very wrong na shetani amewafumba. kwa kawaida, wanatakiwa kwendana na tamaduni zetu sisi hapa tz,kwasababu hawaishi kisiwani, wanaishi kwenye jamii ya watu ambao majority yao hawaamini hivyo...shetani amechafua hii dunia kwa kiwango cha kutisha, ni rahisi sana watu kudanganyika na kuona kama wanafanya mambo ya kawaida tu, na hata hawaoni ubaya wake, kumbe the devil has blinded them. Mungu, Saidia kizazi hiki watu wako wapone! Halelujah to the Lamb of God, who takes away the sins of the world! Amina.
kwa kumalizia, desturi na tamaduni ambazo haziendani na Neno la Mungu are excluded from the above explanation, hapa naongelea tu mambo ya jamii ambayo si kinyume na Neno la Mungu.