hahaha, namshukuru Mungu hivyo vyote ninavyo, lakini sio kwa uwezo wangu, ni kwa neema ya Mungu tu. ndugu yangu, usimdharau mtu hapa duniani, kuna watu wana majumba hata kumi na magari ya kutosha na ya garama, lakini hawawezi kuyatumia...kuna jamaa namfahamu ni tajiri sana, alikuwa na kuburi kama wewe, alipata ajali ni mtu wa kulala tu. nyumba kauza karibia anamaliza zote ili akatibiwe mara india, mara ulaya na watoto amezaa wengi wanasubiria afe lini waanze kugombania. unaweza kuwa na gari usiweze hata kushika usukani, unaweza kuwa na nyumba usiweze hata kulala ndani yake kwani utakuwa unalala hospitalini muda wote tena peke yako ICU...wakati asiye na kitu analala na mke wake home kwenye nyumba ya kupanga ana furaha zote pamoja na kwamba anapanda daladala. hivyo don't define life kwenye vitu kwasababu kuna watu wana vitu lakini hawana furaha ya maisha wengine hadi wanajiua....wakati mamangu kule kijijini ukimwambia kuna tajiri mmoja mkubwa sana amejiua anakushangaaa kwamba alikuwa na shida gani kwani kama nyumba anzo, kama hotel anazo, kama magari anayo ana kila kitu lakini ndio hivyo hana furaha wala amani. definition ya life sio ya kukurupuka. tema mate chini. na si ajabu ndio mara yako ya kwanza leo kununua gari, wakati wenzio hayo magari tumeendesha miaka mingi sana na hatudharau wasio nacho.