Mwanaume asie na gari wala nyumba

Mwanaume asie na gari wala nyumba

Akiwa navyo, asipokuwana navyo unanufaika nini au unapungukiwa na nini?.

NB: Acha umbea jali mambo yako.
 
Hiyo ndo shida yawatu waliotafuniwa na wazazi wanajisahau sana kumbuka mtoa riziki ni Mungu kupata na kukosa yote ni majaliwa.
Maisha ni safari .........
Pia hakuna atakae ishi milele huku duniani na hakuna atakaye zikwa na mali zake tutaviacha vyote.
Acha ushamba na ulimbukeni dharau zitakuponza kn wenye nazo zaidi yako lakini hawamdharau mtu
 
anajiskia kama unavyojiskia wewe si mwenzakoo naye hana gari a
kama wewee
 
Dah wanawake bana kwenye maisha wanawaza Gari tu na nyumba ...ndo maana wanaishia kutanuliwa malinda kwa kupenda vinavyowazidi[emoji23]
 
Kila shetani na buyu lake, kwako we we gari na nyumba vina thamani ila kwangu laaa!
 
Kuna jamaa zangu wananyumba kalii na magari makali ila madeni yao nayo makalii na ndiyo hapo mke anapokimbia anamuachia mwenzie msala.. mi napanda mwendo kasi tu inatosha mkoani napanda bus luxury 35.000/=
Nyumba ninayo ila siyo hekalu yakunitosha mimi tu na mke wangu na mwanangu sitaki wageni wengi
 
hahaha, namshukuru Mungu hivyo vyote ninavyo, lakini sio kwa uwezo wangu, ni kwa neema ya Mungu tu. ndugu yangu, usimdharau mtu hapa duniani, kuna watu wana majumba hata kumi na magari ya kutosha na ya garama, lakini hawawezi kuyatumia...kuna jamaa namfahamu ni tajiri sana, alikuwa na kuburi kama wewe, alipata ajali ni mtu wa kulala tu. nyumba kauza karibia anamaliza zote ili akatibiwe mara india, mara ulaya na watoto amezaa wengi wanasubiria afe lini waanze kugombania. unaweza kuwa na gari usiweze hata kushika usukani, unaweza kuwa na nyumba usiweze hata kulala ndani yake kwani utakuwa unalala hospitalini muda wote tena peke yako ICU...wakati asiye na kitu analala na mke wake home kwenye nyumba ya kupanga ana furaha zote pamoja na kwamba anapanda daladala. hivyo don't define life kwenye vitu kwasababu kuna watu wana vitu lakini hawana furaha ya maisha wengine hadi wanajiua....wakati mamangu kule kijijini ukimwambia kuna tajiri mmoja mkubwa sana amejiua anakushangaaa kwamba alikuwa na shida gani kwani kama nyumba anzo, kama hotel anazo, kama magari anayo ana kila kitu lakini ndio hivyo hana furaha wala amani. definition ya life sio ya kukurupuka. tema mate chini. na si ajabu ndio mara yako ya kwanza leo kununua gari, wakati wenzio hayo magari tumeendesha miaka mingi sana na hatudharau wasio nacho.
Yeah mr Hute; umetiririka vizuri sana nime LIKE ila mleta maada hakuwa na nia mbaya ya kudhalilisha mtu ni kukumbushana tu kujipanga katika maisha.
 
Uanaume siyo kumiliki gari au nyumba!

Kikubwa kutimiza wajibu....
 
Back
Top Bottom