Mwanaume kama mwanamke

Mwanaume kama mwanamke

Lindongo

Member
Joined
Apr 9, 2012
Posts
83
Reaction score
16
Hivi jamani inakuwaje sikuhizi vijana wengi kupenda mabinti walioajiriwa? Mara nyingi vijana hawa shule ni ndogo na wanawadanganyika mabinti kuwa wanafanya na kumiliki biashara kubwa zinazowaingizia kipato wakati sio kweli. Muda mwinigi hushinda kijiweni. wakisha wapata mabinti hao basi wao ni kula kulala. binti aende kazini yeye yupo tu nyumbani. tabia mabay walionayo ni ku-divert namba za simu za wapenzi wao ili wafahmu wameongea nani siku, wanaiba PASSWORD za email za wapenzi wao, na PIN namba za ATM. wanawashawishi waombe mikopo kwenye mabenki ili wafanye biashara, lakini fedha hiyo huishia kufanyia starehe. Kama hiyo haitoshi wanawazuia wapenzi wao kutosaidia ndugu zao hata wadogo zao utadhani pesa ni zao au wao ndio waliwasomesha. matokeo yake ni mabintihawa kuishi maisha ya utumwa wa mapenzi kwa kuwatumikia manaume/ au wapenzi wao.hivi huu kweli ni uungwana?
 
. Mara nyingi vijana hawa shule ni ndogo na wanawadanganyika mabinti kuwa wanafanya na kumiliki biashara kubwa zinazowaingizia kipato wakati sio kweli

binti atakayedanganywa na jamaa wa sampuli hiyo na yeye atakuwa bwe'ge
 
Loh! mwanamme wakuka kijiweni mie wa nini anipishe mie staki mwanamme suruali au magumegume.....
 
Pole kwa yaliyokukuta...nimeipenda stail yako ya uwasilishaji mada..kama shaban robert vile.
 
mmmh, nadhani kama ulivyo sema tatizo ni shule na akili, na nadhani huyo binti nae atakaekuwa anatazwa kusaidia ndugu zake au kurubuniwa na mvulana wa namna hiyo nae atakuwa ana matatizo ya akili pia.
 
Kama huyo mwanamke mwenyewe ameridhika na hayo waliyokubaliana na hicho kidume chake, sioni sababu ya sisi wengine kuingilia mambo yao ya ndani.
 
BAK BAK, tafadhali naomba chaguo la msikilizaji leo uniwekee ule wimbo wa lady jay dee, wanaume kama mabinti.
Natanguliza shukrani za dhati
 
Last edited by a moderator:
wanaume wa siku hizi wanapendwa kulelewa.....

Ila mwanamke anayekopa hela anampa 'boifrendi' loh..........pole yake sana ni kuwa yupo desparate au ni nini?
 
Kama una akili timamu mtu wa aina hii wa nini?Lakini ngoja niwaachie wanawake mtanange wao huu!
 
Mwanamme wa kijiweni wa nini? atawafundisha nini watoto zaidi ya uzembe,ah babu wee mwanamme kazi japo awe na mshahara mdogo.lakini asubuhi mke anakwenda kazini mume umelala huna baisha nzuri wala mbaya mzigo wa nini bora ule yatima kuliko mashaka hayo...
 
mtu hata ukiwa in so called ''love'' lazima uwe na akili ya ziada..yani mtu ashinde kijiweni nimpeleke wapi..nitaanzaje kuchukua mkopo kwa ajili ya mwanaume tustarehe??
Hao mabinti wa kiume sina mcheche nao kabisa. Mwanaume kuwajibika hata kama ni ''good for now'' type..
 
Embu nieleweshe ndugu yangu kwa nini heading yako ni mwanaume kama mwanamke?
 
Wanaume kama mabinti ndio style siku hizi....tembelea Love Connect kuna wengine wameweka mabango kule
 
Embu nieleweshe ndugu yangu kwa nini heading yako ni mwanaume kama mwanamke?
 
kwanza umewadhalilisha wanawake kuwafananisha na wanamme wa aina hiyo, watake radhi.

Pili anayerubuniwa na mwe.hu, nani mwe.hu zaidi?
 
Mwanaume wa aina hiyo ni sawa na kubeba gunia la mavi, lisipokushinda kwa uzito litakushinda kwa harufu
 
mmmh hao wanataka hao wnaume wafanye hivyo na sio kurubuniwa kama umekopa,umetoa namba siri mwenyewe hapo si kurubuniwa?
 
la hasha!!!...huu si uungwanaaaa..
 
BAK BAK, tafadhali naomba chaguo la msikilizaji leo uniwekee ule wimbo wa lady jay dee, wanaume kama mabinti.
Natanguliza shukrani za dhati

Best King'asti, I have tried my level best to search for your request but without any success....SORRY!


 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom