SI KWELI Mwanaume kufanya mapenzi mara mara inasababisha kupata ugonjwa/kansa ya tezi dume?

SI KWELI Mwanaume kufanya mapenzi mara mara inasababisha kupata ugonjwa/kansa ya tezi dume?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na huyu bibie anajaribu kufafanua kuwa wanaume wanaofanya ngono mara kwa mara wapo kwenye hatari kubwa ya kupata Tezi Dume, hii uhalisia umekaaje?

1787293098995.png
 
Tunachokijua
Hakuna ushahidi kwamba kufanya mapenzi au kufika kileleni mara kwa mara husababisha kuongezeka kwa tezi dume (Benign Prostatic Hyperplasia - BPH) au saratani ya tezi dume. Na hakuna sababu ya kuepuka ngono kwa hofu hiyo.

Muhimu zaidi ni kufahamu dalili za mabadiliko ya mfumo wa mkojo na kujadili afya ya tezi dume na mtoa huduma wa afya kadiri umri na vihatarishi vinavyoongezeka.

Baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa wanaume wanaoripoti kumwaga manii mara kwa mara wanaweza kuwa na hatari ndogo ya kupata saratani ya tezi dume, ingawa ushahidi huu haujathibitisha moja kwa moja kwamba kufanya mapenzi au kufika kileleni mara kwa mara huzuia saratani.

Kwa mfano, utafiti mkubwa wa wanaume zaidi ya 31,000 uliona kiwango cha chini cha saratani ya tezi dume miongoni mwa wanaume walioripoti kumwaga manii mara kwa mara. (PubMed)

Kihatarishi kikubwa zaidi cha saratani ya tezi dume ni umri. Hatari huongezeka kadiri mwanaume anavyozeeka. Historia ya familia ya saratani ya tezi dume pamoja na uwepo wa vinasaba (genes) vya saratani pia huongeza hatari.

Wanaume wenye asili ya Kiafrika wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya tezi dume kuliko baadhi ya makundi mengine. (Cancer.gov). Uvutaji sigara pia umehusishwa na saratani ya tezi dume, hasa kwa upande wa ugonjwa mkali (advanced stage) na hatari ya kufariki kutokana na saratani.

Ni muhimu kuzungumza na mtoa huduma wa afya kuhusu uchunguzi wa saratani ya tezi dume, ambao unaweza kuhusisha kipimo cha damu cha PSA (Prostate-Specific Antigen) na, inapofaa, uchunguzi mwingine. Uchunguzi unapaswa kuzingatia umri, historia ya familia, asili ya kinasaba na faida pamoja na madhara yanayoweza kutokea kutokana na uchunguzi. (USPSTF)
Tezi dume ni kiungo kila mwanaume anacho. Ukifika umri fulani kitaongezeka ukubwa ,, ukubwa ukizidi ndipo changamoto inaaza. Kinaweza kupata saratani pia. Kufanya mapenz mara kwa mara kunaweza kwanamna fulani kupunguza uwezekano lakini sio tiba ya kuzuia
Mimi haya mambo ya mitandaoni sometimes huwa naona waduwanzi tu kwasababu nimesikia mara nyingi sana kama mwanaume anashiriki tendo mara kwa mara anakuwa anapunguza risk ya kupata hilo tatizo huyo nae anakanusha.
 
Mimi haya mambo ya mitandaoni sometimes huwa naona waduwanzi tu kwasababu nimesikia mara nyingi sana kama mwanaume anashiriki tendo mara kwa mara anakuwa anapunguza risk ya kupata hilo tatizo huyo nae anakanusha.
Kwanza hakuna ugonjwa unaoitwa Tezi Dume!!!! Kuna uvimbe au kansa ya Tezi Dume. Kila mwanaume ana Tezi Dume
 
Kwa uelewa wangu tezi dume tunaita tu ila ni kansa ya tezi dume au uvimbe wa tezi dume, tezi dume ni kiungo sio ugonjwa!

Kufanya mapenzi sana, kumwaga kunaweza kuongeza uwezekano wa kupata tezi dume, lakini pia kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata tezi dume. Itategemeana na BMI ya mtu,mtindo wake wa maisha ulaji, mazoezi, stress, na vinasaba.
 
Johnny sins anatezi dume ?

Nadhani Inategemea unafanya mapenzi mara kwa mara na Nani, unakula na kuuweka mwili wako kwenye mazingira gani inachangia pia .
 
Acha Uoga Kuna Magonjwa Yanaitwa Ya Uzeeni.

Jitahidi Kuwa Na Discipline Kwenye Lifestyle Yako Ukiwa Kijana.

Kila Kitu Fanya Kwa Kiasi.
 
Wakuu nimekutana na huyu bibie anajaribu kufafanua kuwa wanaume wanaofanya ngono mara kwa mara wapo kwenye hatari kubwa ya kupata Tezi Dume, hii uhalisia umekaaje?
View attachment 3654111
View attachment 3654112
Having sex or ejaculating frequently does not cause prostate cancer. In fact, large health studies show that men who ejaculate more often—such as 21 or more times a month—may have a slightly lower risk of getting prostate cancer compared to men who ejaculate less often...
 
Bora hata leo mna clinic yenu wanawake tupumzishwe😎
Clinic yetu, mada za wanawake zimekuwa nyingi sana humu jukwaani na hiyo ndo inathibitisha kweli kuwa wanawake ni special group
 
Back
Top Bottom