Mwanaume kuiomba airtime voucher!!!!

Naomba kuuliza kabla sijachangia.

Watu tuliozaliwa zamani tunaruhusiwa kuichangia hii thread?

Nilisahau kuwasalimu: Marahaba wajukuu zangu.

Karibuni kitandani tulale
 
Masharobaro wamejaa siku hizi mpaka maofisini mtu anakukamia namna hiyo haoni haya ina maana pesa zako wewe hazina kazi zake ndio zina kazi sana au?mwehu huyo. mwanamke kubembelezwa na vizawadi vya hapa na pale, kumpa vocha na zawadi nyingine mwanaume wako ni mwenyewe uamue sio akupressurise.kimbia hilo ni zigo la mavi litakunukia tu hata ulizibe na nini
 
Naomba kuuliza kabla sijachangia.

Watu tuliozaliwa zamani tunaruhusiwa kuichangia hii thread?

Nilisahau kuwasalimu: Marahaba wajukuu zangu.

Karibuni kitandani tulale

Tena nyie ndio mnafaa sababu ndio mnaojuwa kulea wasichana,kubembeleza na mengineyo. eti na wewe mpaka uombwe ndio umpe msichana wako au unajihisi wewe ndio mwenye jukumu la kumfanyia mambo kama hayo?
 
kwani kuna tatizo gani kila mtu ana mtazamo wake katika kuingia kwenye mahusiano lakini kuwa makini mara nyingi watu wanamna hiyo mpaka kwenye ndoa wana matatizo utapewa kuwa baba shauri yako nshakuambia byeeeee.
 
naona nazeeka sasaaaa
bwana nazeeka sasaaaa

Prof J featuring Mr II
 
mh! Hivi vyuo vya short courses vilivyojaa hakuna wanaotoa course ya kutongoza? Ningemlipia akajifunze strategies. Akajipange bwana mizinga mapema hivi!
 
Tena nyie ndio mnafaa sababu ndio mnaojuwa kulea wasichana,kubembeleza na mengineyo. eti na wewe mpaka uombwe ndio umpe msichana wako au unajihisi wewe ndio mwenye jukumu la kumfanyia mambo kama hayo?

Sisi tuliozaliwa zamani na kufuata misingi imara ya mamabu zetu:

1. Ni marufuku kumbomu binti bila kujali unatongoza au unachumbia
2. Binti akikupa hela kwa hiari yake wakati unamtongoza, unapaswa kuikataa ili kuuthibitisha uanaume wako
3. Ni marufuku kumwomba hata mkeo hela.....sanasana labda 'umkope kimagirini'

I mean mwanamke kumpa hela mwanaume enzi zetu ilikuwa ni udhalilishaji. Anachotakiwa mwanamke kumpa mwanaume ni vijizawadi bana, siyo hela.

Hivi hii thread tunajadili nini vile?
 
Hapa mnadiscuss nini?
Mwaume kuomba Vocha?
Mwanaume kuomba vocha wakati anatongoza?
Mwanaume kuomba vocha baada ya kutongoza na kukubaliwa?
Mwanaume kuomba vocha pale tu anapokua na shida?

Ntarudi!!
 
huna utu......huna staha.....huna adabu.....ndio niny mnaopigania haki sawa?......anakosa nini kukuommba voucha....wewe vipi?

wapendanao wanasaidiana......... umenishangaza kweli
 
huna utu......huna staha.....huna adabu.....ndio niny mnaopigania haki sawa?......anakosa nini kukuommba voucha....wewe vipi?

wapendanao wanasaidiana......... umenishangaza kweli
Chonde chonde na hiyo komputer yangu usiniharibie keyboard bana, naona unazigonga kwa hasira si mchezo! subiri ya kwako itoke kwa fundi bana!!
 
We dada ni vile tu hujampenda huyo kaka lakini ingekuwa kwamba roho yako imemkubali walahi ungempa hiyo voucher. mbona sioni tatizo???

wewe ndo umesema kweli...huyu ni mmoja wa kina dada ukimuoa uzee wako unakuwa wa manung'uniko.......hajampenda kwa dhat......na anayonyesha jisi gani alivyo.... ama kweli MIAFRICA NDIVYO ILIVYO!
 
Babu Asante
Afadhali umekuja mana watu wananiona mie nambania
mtu ndo kwanza anatongoza hapo hajakubaliwa ye anaanza na vibomu
inakuja kweli hii
 
Chonde chonde na hiyo komputer yangu usiniharibie keyboard bana, naona unazigonga kwa hasira si mchezo! subiri ya kwako itoke kwa fundi bana!!

kuna ile moja imemwagikiwa chai asubuhi......nikaweka stoo na kuvuta hiki kitu......kii bod yake bado mpyaaaa:focus:

umemuoaa huyu dada alivyo...maada ya ajabu kabisa hii
 
Guys me i like this approach. Usipate kichefuchefu banaa.. Mtu mzima anataka kujua kama kweli una mwelekeo wa kumpenda, coz wanawake hamuaminiki bana, leo unakataa tena mbele ya umma then kesho unampenda tena kwa machozi!!!

Anyway nawatakia kila la kheri........
 
huna utu......huna staha.....huna adabu.....ndio niny mnaopigania haki sawa?......anakosa nini kukuommba voucha....wewe vipi?

wapendanao wanasaidiana......... umenishangaza kweli

Edson taratibu naona hukuelewa kinachoongelewa naomba urudie kusoma mada tafadhali..
angekuwa mpendanao wangu nisingekuja jamvini kusema..ushanpata?
kijana ndo anatupa ndoano na nishamwambia simtaki nina wangu,lakini bado anaomba vocha na kunambia pls call me back
hapo nimekosea nini..
endelea kushangaa..
 
Hapa mnadiscuss nini?
Mwaume kuomba Vocha?
Mwanaume kuomba vocha wakati anatongoza?
Mwanaume kuomba vocha baada ya kutongoza na kukubaliwa?
Mwanaume kuomba vocha pale tu anapokua na shida?

Ntarudi!!

Kimey..jibu ni hapo kwenye red
 
kuna ile moja imemwagikiwa chai asubuhi......nikaweka stoo na kuvuta hiki kitu......kii bod yake bado mpyaaaa:focus:

umemuoaa huyu dada alivyo...maada ya ajabu kabisa hii

Inaelekea we ndo haohao tunaowaongelea mnapenda miteremko hali hamjakubaliwa na ndo mnajiharibia sasa mana mwanamke hawezi kukukubali kwa style hii.badilika kijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…