King Jody
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 1,834
- 3,456
Wakati mwingine ni kweli wanakuwa na maneno ya kuudhi au kwa lugha nyingine unaweza kusema wana mdomo,
Kamwe huwezi kumbadilisha mwanamke tabia kwa kipigo, ni mtu mzima amelelewa kwao na wewe umelelewa kwenu mmekutana ukubwani, kila mtu na tabia yake.
Tafuta njia mbadala ya kukaa naye na kuzungumza kwa upendo, ni mtu mzima atakuelewa japo wapo ambao ni pasua kichwa, hawasikii wala hawaelewi, utapiga utaua bure.
Mwanake siyo mtoto mdogo eti umbadilishe tabia kwa kipigo, akiamua kutulia atatulia mwenyewe, tumia hekima na busara badala ya kipigo.
Mpende, mjali, mdekeze pale inapobidi na kumheshimu, mpige kwa maneno mazuri mf. wewe ni mwanamke mrembo kliko wote Duniani, msifie, mtamkie neno nakupenda mara kwa mara.
Biblia Takatifu inatuambia tuishi nao kwa kutumia akili. soma 1.Petro 3.7 Kadhalika enyi wanaume. Kaeni na wake zenu kwa akili: na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu:
Nb. Amani na upendo vikae nanyi siku zote.