Mwanaume; Kuna wakati muambie Mmke wako kwaheri, ukubali kuwa yameisha!

Mwanaume; Kuna wakati muambie Mmke wako kwaheri, ukubali kuwa yameisha!

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Mwanaume, nikukumbushe tu, kiasili hatujaumbwa kuvumilia, yaani ile hisia ya uvumilivu tunakuwa hatuna kabisa, ndiyo tulivyoumbwa.

Kama ukishaona mke wako anaanza kukufanyia dharau, iwe ni sababu ya kipato au kwa sababu tu anaona ameshakuzoea, kama mke wako umeshaanza kukufumania na wanaume wengine, analala nje bila sababu na anakujibu vibaya, kitu cha uanaume ni kumuacha aende zake!

Ninarudia, kitu cha uanaume ni kumuacha aende zake! Kama mna watoto, mlee watoto, mambo ya kuitana vikao, mambo ya kumlilia abadilike hayawezekani. Kuna hasira iliyoko ndani ya moyo wako ambayo hata huijui, siku ikitoka, utakuja kujilaumu maisha yako yote!

Anaweza kukufanyia kitu kibaya hadi ukisimuliwa unashangaa mimi ilikuwaje nikafanya hivi? Wakati huo uko jela au sijui wapi, lakini tayari umeshaharibu maisha yako!

Najua watu mtasema, "Kwa nini unaongelea wanaume tu, inamaanisha wanawake wanatakiwa kuvumilia?"

Hapana, simaanishi hivyo, ila wanawake hawana ile hasira tuliyonayo sisi wanaume, imejificha sehemu!
Mwanamke anaweza kumfumania mume wake asubuhi, mchana akanunuliwa iPhone, akasahau kila kitu na kupost picha ya furaha, akimrusha roho mchepuko.

Lakini mwanaume, ukishajua mke wako analiwa, ni ngumu hata kuongea naye, hata kumwangalia ni ngumu!
Na wewe mwanamke, ukiona unamfanyia mume wako mambo haya:

Unamtukana

Unatembea na wanaume wengine lakini haongei

Mume wako amekufumania na badala ya kuchukua hatua, anakwenda kwa wazazi kuomba suluhu
Usijidanganye kuwa umemshinda, ondoka mwenyewe!

Najua unajisifu, "Mume wangu ana uvumilivu hakohoi kwangu," lakini wanaume wana kiwango cha ujinga kinachovumilika. Suala ni muda tu, ile hasira itatoka na familia yako ndiyo itaumia zaidi.

Kama umemchoka mwanaume, muache! Usichepuke eti unalipiza kisasi, sisi wanaume hatuna mshipa wa msamaha!
 
...kataa ndoa wake mbele kwa goli 4-0
Gooal...Namna gani pale wanapata goli la 5.
 
Back
Top Bottom