SI KWELI Mwanaume kunyonya matiti ya mwanamke husaidia kupunguza hatari ya Saratani ya matiti kwa mwanamke

SI KWELI Mwanaume kunyonya matiti ya mwanamke husaidia kupunguza hatari ya Saratani ya matiti kwa mwanamke

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu katika pitapita mtandaoni nimekutana na hoja ambayo hata mtaani nimekuwa nikikutana nayo kwamba mwanaume kunyonya matiti ya mwanamke husaidia kupunguza hatari ya kansa ya matiti kwa mwanamke. uhalisia wa hili ni upi?
breasts.jpeg
 
Tunachokijua
Kansa ya matiti ni aina ya kansa ambayo huanza kadri ya ukuaji wa seli katika tishu za matiti. Kansa hii mara nyingi imekuwa ikiwakumba wanawake zaidi ukilinganisha na wanaume japo yeyote anaweza akapatwa na ugonjwa huu.
ds00328_-ds00771_-wo00031_im03982_w7_nipplechangesthu_jpg.jpg


Zipo sababu kadhaa ambazo zinaweza kusababisha ugonjwa huu ikiwemo, kuwa na familia yenye historia ya kuwa na ugonjwa huu, kuwa na historia binafsi ya kuwahi kukumbwa na ugonjwa huu mfano mtu aliyewahi kupata kansa ya titi la upande mmoja ipo hatari pia ya kupatwa katika titi la upande wa pili, kuanza kwa hedhi katika umri mdogo mfano chini ya miaka 12, utumiaji wa vilevi, kupata mtoto katika umri mkubwa na kadhalika.

Kumekuwapo na madai kuwa unyonywaji wa matiti ya mwanamke wakati wa faragha na mwanaume kunapunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya matiti.


Je uhalisia ni madai hayo ni upi.

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ambao umepitia tafiti mbalimbali umebaini kuwa si kweli kwamba mwanaume anaponyonya matiti ya mwanamke wakati wa faragha kunaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya matiti.

Tafiti zinaeleza kuwa unyonyeshaji unaozalisha maziwa (mama wenye watoto) ndiyo husaidia kupunguza hatari ya kukumbwa na ugonjwa huo tofauti na kitendo cha unyonyaji kinachofanywa na mwanaume ambacho hakizalishi maziwa huku kikiwa hakina msaada wowote katika kuondoa hatari ya kupata ugonjwa huo. Hivyo wanawake wanashauriwa kunyonyesha watoto wao kwa muda mrefu ili kusaidi kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa huo.

Wakati mwanamke ananyonyesha, mabadiliko ya kawaida ya homoni yanaweza kuchelewesha hedhi, jambo ambalo husababisha viwango vya oestrogen kuwa chini. Oestrogen inaweza kuchangia ukuaji wa seli za saratani ya matiti.

Tovuti ya Mayo clinic inaeleza kuwa endapo mwanamke akiwa ana mtoto mdogo, kunyonyesha kunaweza kusaidia katika kuzuia saratani ya matiti. Kadri unavyonyonyesha kwa muda mrefu, ndivyo ambavyo uwezakano wa kujikinga unaweza kuongezeka.

Kulingana na utafiti uliofanywa na Cancer Research UK ambao ni uchambuzi wa kina wa tafiti 47 zilizochapishwa, zikiwa na takriban washiriki 150,000 kutoka nchi 30 ikibainika kuwa kunyonyesha kunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya saratani ya matiti,

Kwa mujibu wa tovuti ya prime progress ambayo inamnukuu Dk. Usha Anenga daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka nchini Nigeria ambaye anafafanua uhalisia juu ya madai ya mwanaume kunyonya matiti kwamba itapunguza hatari ya saratani ya matiti ambapo mtaalamu huyu anakanusha hoja hiyo.

"Ni kunyonyesha maziwa ya mama kwenda kwa mtoto ndiko kunakopunguza hatari ya saratani ya matiti, sio tu wanaume wazima kunyonya matiti bila maziwa kuzalishwa,"

Athari ya kinga inatokana na mabadiliko ya homoni wakati wa uzalishaji wa maziwa na kunyonyesha, ambayo, kama alivyoeleza Dk. Anenga, husaidia kudhibiti tishu za matiti na hivyo kupunguza hatari ya kupata saratani. Kunyonya matiti bila muktadha wa kunyonyeshaji unaotokana na maziwa yaliyozalishwa hakutoi matokeo yanayofanana.

Ili kupunguza hatari ya kukumbwa na ugonjwa wa saratani ya matiti inashauriwa kuepuka unywaji wa pombe uliokithiri, uvutaji wa sigara, kudhibiti uzito wa mwili unaopitiliza, punguza matumizi ya tiba ya homoni baada ya kukoma kwa hedhi, pamoja kufanya mazoezi ya mwili.

Mara unapobaini mabadiliko yoyote katika sehemu ya titi vi vema kumuona daktari kwa uchunguzi na ushauri zaidi.​
Ikithibitika kuwa kweli, wanaume tutajiongezea ajira chapu.
 
SAWA
Kunyonyesha Maziwa Mtoto Ndiyo Kunakosaidia
 
Back
Top Bottom