Mwanaume mpende mke wako

Mwanaume mpende mke wako

Innovator97

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
274
Reaction score
375
UMEOA? Jivunie mkeo/mwanamke wako, 'Feel Proud Of Your WIFE' na kamwe usione hatari kumsifu mbele ya Macho yake, usijiulize mara MBILI kusema "NAKUPENDA MKE/MPENZI WANGU MZURI"

Tambua, amefanya maamuzi ya kusafiri na wewe kwenye safari ndefu ya maisha; hakuona mwingine huko pembeni ambaye angeweza kutembea katika safari hiyo, isipokuwa wewe, Mume wake.

Ameacha ndugu zake wa damu, sio kwa sababu wewe ni ndugu yake zaidi ya wengine, hapana, kwa sababu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya kwanza ya watu wake wa muhimu zaidi. Anaishi na wewe sasa.

Ameamua kumuacha mama yake aliyembeba tumboni, akaleta ulimwenguni, akamlea na kumnyonyesha maziwa yake, amemuacha baba yake pia, ameamua kukufuata wewe mume wake.

Ameamua kuwa sehemu ya maisha yako, ameachana na marafiki zake huko, sasa wewe ndie ambaye utampangia ratiba zake, utamulekeza na kumfahamisha namna sahihi nyingine ya kuishi, Wewe mumewe!

Alipokuwa kwao, alikuwa na aina ya vyakula ambavyo alikuwa akivipenda, ameishi akivitumia lakini sasa yupo kwako, analazimika kupenda chakula ambacho wewe (mumewe) unapenda, unachagua kula nini, nae atakula!

Ameamua kuchanganya matamanio yake na yale ambayo wewe (mume wake) unapenda. Atalazimika kupenda hata kutazama Mpira wa miguu, wakati Mwanzo hakuwahi kuwa shabiki kabisa.

Umemuoa sasa, hakutumikii wewe pekee, anawatumikia hadi wazazi wako. Kuna wanaume wakioa, wanaendelea kuishi kwao, hivyo mwanamke huyu atalazimika kuwa sehemu ya shughuli za nyumbani kwenu.

Atashiriki kwenda shamba, atashughulika kupika na kufanya shughuli za nyumbani kwenu, chakula atakachopika, watakula wazazi wako, wanao na wewe pia. Mkeo, ameamua kuwatumikia!

Mama watoto wako huyu. Amekubali kubeba mtoto/watoto wako tumboni miezi tisa. Huyu ni mtu wako muhimu. Sio kila mwanamke anaweza kukubali kuwa mama wa watoto wako, mshike huyu, usimuache aende zake!

Mkeo, Pamoja na kwamba anao ndugu zake wa damu kwao, lakini kwenu atawajibika kuwapenda kaka na dada zako, atawajibika kuwaonesha upendo wa dhati machoni, kwa matendo, atafanya yote haya, kwa ajili yako.

Mkeo, ndie rafiki yako wa kwanza, ndie ambaye anabeba siri zako za ndani na nje na kuziona kama zake. Anawajibika kuwa rafiki yako 'by-defaults' na atapaswa kuwa rafiki mwema! Mkeo ni swahiba wako nambari-wani!

Mara nyingine, mwanamke huyu atasahau au kukosa kabisa muda wa kujitazama na kujali mahitaji yake, kwa sababu muda mwingi anautumia kuifanya familia yake (wewe mume wake ukiwepo) kuwa na furaha na amani.

Anachukua jukumu la kuwatunza wanao. Atawapa mahitaji yote. Atawapikia chakula, atawafulia nguo, atawapikia chakula, atawabembeleza walale, atawasaidia 'homework' na asubuhi atawaamsha kwenda shule.

Kama wazazi wako wapo nyumbani kwako, aidha wanaishi hapo au wamekuja kusalimia, mkeo Anawajibika kuwashughulikia na kuwahudumia, wapate mahitaji ya lazima kama KULA na KULALA..

Fikiria wewe ndie ungelikuwa katika nafasi yake na uone kwa jinsi gani ingelikuwa ngumu. Pamoja na yote hayo magumu, anawajibika kuwa na furaha muda wote, maana anaogopa kuonekana ni watu mwenye kumiliki KIBURI.

Wakati mwingine ameumizwa. Ndio! Wakati mwingine amekerwa sana na mambo kadhaa kwenye familia yako au kutoka kwako, lakini anawajibika kuwa na furaha usoni, anaogopa kuonesha hadharani, ana hofu kukupoteza!

Wanawake wengi wanapoumizwa, wanaamua kubaki kimya, wanakaa kimya. Sio kwa sababu wanapenda kuwapa adhabu waume zao, laa! Hasha, wanajukumu la kulinda ndoa zao, wananyamaza kimya!

Wanayo hofu, wanawake wengi wanaishi kwa hofu hata wakipata maumivu, hutulia kimya, maana kwa hasira wanaweza kuongea maneno makali ambayo baadae watayajutia na hata kuharibu mahusiano yao.

Anatakiwa kuwapenda wadogo kwenye familia na anatakiwa kwa wakati huo kuwapa heshima kubwa watu wazima kwenye familia yako. Anatakiwa kuwatumikia wewe na familia yako, kiwa sehemu yenu.

Sasa, ni wakati wa kufikiri kumfanya mkeo kuwa MALKIA sio kufikiri jinsi ya kumuudhi na kumkera. Muoneshe unamjali. Mfanye kipaumbele chako sasa.

"Try the knight-in-shining armor bit instead of the i-know-I'm-in-the-doghouse bit. But take a 'risk' and slay a few dragons and kill a few spiders and take out the trash... Not in apologetic way, but in a "you're my princess" way"

Hii ni falsafa ya 'kiskotishi' katika mapenzi. Wanaume tuitumie sasa! Tujivunie kuwa na watu hawa katika maisha yetu, tuwafanye kuwa 'wapendwa' wetu sio watumwa wetu!

Mkeo, hadi kutoka kwao, ameamua kuwa nawe kwa dhati kabisa ya moyo wake (sio wote katika eneo hilo), ukipata mke mwema, umebahatika, shukuru maana sio wote wenye bahati kama yako!

@C$P MMM
 
hakuona mwingine huko pembeni ambaye angeweza kutembea katika safari hiyo, isipokuwa wewe, Mume wake.
Mkuu wanawake ni opportunists (wanaangalia fursa/future/kibunda)

Iko hivi huenda kuna jamaa aliwakubali kuliko wewe lakini hawakuvutiwa naye wamuoe

Ila amekuchagua wewe ameona una afadhali akilinganisha na wengine waliobaki kwenye circular dating yake

Wanawake wengi siku hizi wanaolewa na wanaume wasiowapenda kuna wakati umri ukisonga au akiwa single maza anamkubali mwanaume ili mradi tu na yeye atambe ameolewa
 
Ameacha ndugu zake wa damu, sio kwa sababu wewe ni ndugu yake zaidi ya wengine, hapana, kwa sababu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya kwanza ya watu wake wa muhimu zaidi. Anaishi na wewe sasa
Maandiko yanasema mwanaume atawaacha wazazi wake na kuungana na mke wake

Mkuu mwanaume ndiye anayechagua mke sio mwanamke ndiye anayechagua mume

Kumbuka mwanaume ndiye anayeamua nani wa kumuoa
 
Paragraph nyiiiiiiiiiiiiiiiiiingiiiiiii ila unaeleza jambo hilohilo tu. Kwann usingeishia aya moja tu kuliko kujipinda kuweka aya nyingi za kurudia maelezo
 
UMEOA? Jivunie mkeo/mwanamke wako, 'Feel Proud Of Your WIFE' na kamwe usione hatari kumsifu mbele ya Macho yake, usijiulize mara MBILI kusema "NAKUPENDA MKE/MPENZI WANGU MZURI"

Tambua, amefanya maamuzi ya kusafiri na wewe kwenye safari ndefu ya maisha; hakuona mwingine huko pembeni ambaye angeweza kutembea katika safari hiyo, isipokuwa wewe, Mume wake.

Ameacha ndugu zake wa damu, sio kwa sababu wewe ni ndugu yake zaidi ya wengine, hapana, kwa sababu amekuchagua wewe kuwa sehemu ya kwanza ya watu wake wa muhimu zaidi. Anaishi na wewe sasa.

Ameamua kumuacha mama yake aliyembeba tumboni, akaleta ulimwenguni, akamlea na kumnyonyesha maziwa yake, amemuacha baba yake pia, ameamua kukufuata wewe mume wake.

Ameamua kuwa sehemu ya maisha yako, ameachana na marafiki zake huko, sasa wewe ndie ambaye utampangia ratiba zake, utamulekeza na kumfahamisha namna sahihi nyingine ya kuishi, Wewe mumewe!

Alipokuwa kwao, alikuwa na aina ya vyakula ambavyo alikuwa akivipenda, ameishi akivitumia lakini sasa yupo kwako, analazimika kupenda chakula ambacho wewe (mumewe) unapenda, unachagua kula nini, nae atakula!

Ameamua kuchanganya matamanio yake na yale ambayo wewe (mume wake) unapenda. Atalazimika kupenda hata kutazama Mpira wa miguu, wakati Mwanzo hakuwahi kuwa shabiki kabisa.

Umemuoa sasa, hakutumikii wewe pekee, anawatumikia hadi wazazi wako. Kuna wanaume wakioa, wanaendelea kuishi kwao, hivyo mwanamke huyu atalazimika kuwa sehemu ya shughuli za nyumbani kwenu.

Atashiriki kwenda shamba, atashughulika kupika na kufanya shughuli za nyumbani kwenu, chakula atakachopika, watakula wazazi wako, wanao na wewe pia. Mkeo, ameamua kuwatumikia!

Mama watoto wako huyu. Amekubali kubeba mtoto/watoto wako tumboni miezi tisa. Huyu ni mtu wako muhimu. Sio kila mwanamke anaweza kukubali kuwa mama wa watoto wako, mshike huyu, usimuache aende zake!

Mkeo, Pamoja na kwamba anao ndugu zake wa damu kwao, lakini kwenu atawajibika kuwapenda kaka na dada zako, atawajibika kuwaonesha upendo wa dhati machoni, kwa matendo, atafanya yote haya, kwa ajili yako.

Mkeo, ndie rafiki yako wa kwanza, ndie ambaye anabeba siri zako za ndani na nje na kuziona kama zake. Anawajibika kuwa rafiki yako 'by-defaults' na atapaswa kuwa rafiki mwema! Mkeo ni swahiba wako nambari-wani!

Mara nyingine, mwanamke huyu atasahau au kukosa kabisa muda wa kujitazama na kujali mahitaji yake, kwa sababu muda mwingi anautumia kuifanya familia yake (wewe mume wake ukiwepo) kuwa na furaha na amani.

Anachukua jukumu la kuwatunza wanao. Atawapa mahitaji yote. Atawapikia chakula, atawafulia nguo, atawapikia chakula, atawabembeleza walale, atawasaidia 'homework' na asubuhi atawaamsha kwenda shule.

Kama wazazi wako wapo nyumbani kwako, aidha wanaishi hapo au wamekuja kusalimia, mkeo Anawajibika kuwashughulikia na kuwahudumia, wapate mahitaji ya lazima kama KULA na KULALA..

Fikiria wewe ndie ungelikuwa katika nafasi yake na uone kwa jinsi gani ingelikuwa ngumu. Pamoja na yote hayo magumu, anawajibika kuwa na furaha muda wote, maana anaogopa kuonekana ni watu mwenye kumiliki KIBURI.

Wakati mwingine ameumizwa. Ndio! Wakati mwingine amekerwa sana na mambo kadhaa kwenye familia yako au kutoka kwako, lakini anawajibika kuwa na furaha usoni, anaogopa kuonesha hadharani, ana hofu kukupoteza!

Wanawake wengi wanapoumizwa, wanaamua kubaki kimya, wanakaa kimya. Sio kwa sababu wanapenda kuwapa adhabu waume zao, laa! Hasha, wanajukumu la kulinda ndoa zao, wananyamaza kimya!

Wanayo hofu, wanawake wengi wanaishi kwa hofu hata wakipata maumivu, hutulia kimya, maana kwa hasira wanaweza kuongea maneno makali ambayo baadae watayajutia na hata kuharibu mahusiano yao.

Anatakiwa kuwapenda wadogo kwenye familia na anatakiwa kwa wakati huo kuwapa heshima kubwa watu wazima kwenye familia yako. Anatakiwa kuwatumikia wewe na familia yako, kiwa sehemu yenu.

Sasa, ni wakati wa kufikiri kumfanya mkeo kuwa MALKIA sio kufikiri jinsi ya kumuudhi na kumkera. Muoneshe unamjali. Mfanye kipaumbele chako sasa.

"Try the knight-in-shining armor bit instead of the i-know-I'm-in-the-doghouse bit. But take a 'risk' and slay a few dragons and kill a few spiders and take out the trash... Not in apologetic way, but in a "you're my princess" way"

Hii ni falsafa ya 'kiskotishi' katika mapenzi. Wanaume tuitumie sasa! Tujivunie kuwa na watu hawa katika maisha yetu, tuwafanye kuwa 'wapendwa' wetu sio watumwa wetu!

Mkeo, hadi kutoka kwao, ameamua kuwa nawe kwa dhati kabisa ya moyo wake (sio wote katika eneo hilo), ukipata mke mwema, umebahatika, shukuru maana sio wote wenye bahati kama yako!

@C$P MMM
Katika yote nimeguswa na ukimya tunapoumizwa au kukasirishwa. Hii ndio aina yangu ya maisha, nikiwa na hasira kupitiliza huchagua kukaa kimya.
Naogopa sana kuongea maana nitashindwa kuyabeba baadae niliyoyasema.
 
Huu uzi wanaume wenzio watakupiga mawe mpk ukome ila message sent 🤣🤣🤣
 
  • Mshangao
Reactions: 511
Back
Top Bottom