MALKIA WA TABASAMU
Member
- May 23, 2024
- 15
- 43
Mwanaume mwenye uhitaji na wanawake wengi, hana furaha na yeye mwenyewe.
Kwake kuwa na usikivu wa wanawake wengi, kunamsaidia kulisha nafsi yake, kuficha kutojiamini kwake.
Huyu mwanamume asiyejiamini, atacheza na hisia za wanawake wengi, huku akidhani ananufaika na kuongeza kujistahi kwake.
Ni hivi!, mwanamume wa kweli hahitaji zaidi ya mwanamke mmoja mzuri machoni pake; ambaye atawekeza muda na nguvu zake kwake.
Mwanaume wa kweli, hujithibitisha kwa kuwajibika na kuishi katika nafasi aliyoumbwa kwayo.
Mwanaume wa kweli hahitaji maelfu ya wanawake kumthibitisha wala kuelezea urijali wake.
Moyo wake hujaa mapenzi, kwa sababu anajipenda na kuyapenda maisha yake. Huyu huwa mtu na nusu.
Hujitambulisha kwa maneno machache na huacha muda uitambulishe kazi yake.
Huongoza maisha yake. Na popote atakapopata nafasi, athari yake chanya' huonekana mapema sana.
Husimama kama shujaa nyakati zote. Hutetea wanyonge, hali mkate wa dhuluma. Wala haongozwi na mihemko.
Sio mfitini, wala mwingi wa masengenyo. Sio mlevi wala tegemezi wa kihisia. Ana hadhi ya kuilinda.
Ni shujaa wa maisha yake mwenyewe. Hilo halimzuii kuthamini michango midogo midogo ya watu wengine kwenye maisha yake.
Anajua kuomba na kushukuru inapohitajika. Anajua kusema na kusikiliza kabla ya kutoa hukumu.
Ameibeba maana ya kichwa, na milango yake yote ya fahamu ajua kuitumia kwa hekima.
NGUVU YA MWANAUME WA KWELI NI MAARIFA AMBAYO HACHOKI KUYATAFUTA.
✍ Kungwi wa kisasa.