Unajua watu tunapenda kupindisha sana ukweli, kumwambia mwanaume mwenzako NAKUPENDA kwangu mimi siyo sahihi. Natoa ushuhuda wa ukweli, ilitokea nilikuwa na jamaa yangu fulani akajitahidi kunizoea na mwisho wa siku akawa ananitumia message tata. Mimi nilipotezea lakini kumbe kupotezea kwangu kulimpa courage kwamba mimi sina shida, jamaa akazidi kuonyesha hisia zake zaidi na ndipo nilipotambua kuwa jamaa si rizki! Nikajipanga kumpa fact, siku nikamwambia tutoke eneo ambalo ni baa pekee nikamuuliza vipi mkuu mbona SIKUELEWI? Akanijibu Mzee wa Rula elewa kama nilivyojielza kuanzia kwenye message hadi leo hii tupo hapa pls nisaidie? Nikamuuliza nikusaidie nini? Akacheka akaniambia MR hilo nalo swali? Anyway ni story ndefu, ila nilihitimisha kwa kumwambia A FRIEND CAN'T KILL HIS FRIEND, nikamnyooshea na kumalizia kuwa jambo hili hutalisikia mitaani, nitafanya kama kiatu kinavyositiri aibu ya soksi. Baada ya kumtema mshikaji akakata mawasiliano na haukupita muda nikamuona amevishwa pete! Basi mpaka leo hii tuna wasiliana nae lakini ameoa tayari na ana mtoto mmoja. YOTE HAYA YALIANZIA KWENYE MIZAH MIZAHA, NAKUPENDA, HALAFU WEWE MR HUKATILI WEWE, MKITANIANA SIKU NYINGINE ANAKWAMBIA IPO SIKU NITAKUPA MIMI WEWE!!! Mambo kama haya si ya kuyafumbia macho, imagine ndiyo angekuwa mwanao anawaambi rafiki zake I LOVE U, ungefanyaje?