Mkuu tulizaliwa tukakaririshwa hivyo sikatai.
Lakini tuliposoma na kuelimika, tukaja gundua kuwa kumbe mahindi (maize meal), yawe ni unga wa sembe ama dona ndiyo chakula chenye thamani ya chini kabisa kuliko vyote katika vyakula vya mazao ya nafaka!
"Food value" ya mahindi hailingani na ngano, mchele, mtama ama uwele.
Na pia hauwezi kulinganisha na vyakula vya mizizi kama mihogo na viazi.
Kwa wazungu huko, mazao ya mahindi ni chakula cha mifugo kuanzia majani na mbegu zake.
Kabla ulimwengu haujastaarabika, kwao mahindi kilikuwa pia ni chakula cha watumwa.
Tukitaka kusifia milo, basi tuchunguze kwanza ni chakula gani tunachoweza kutoka nacho hadharani na kujikisifia kutumia.
Mi nadhani mtu anayekula wali ama chapati ana gain more energy kuliko anayekula ugali.
Ugali kiuhalisia ni chakula cha chini sana na hakina thamani yoyote katika afya ya binadamu.
Kuna baadhi ya nchi hawaelewi kabisa stori za kitu kinachoitwa ugali na wako strong sana ki afya na wanatuzidi wala ugali!