inategemeana, cha kwanza, inategemeana na kosa alilolifanya mkeo...ndo maana hata wanaume kwa wanaume hawapigani hivihivi, inategemeana na kosa alilolifanya opponent wako. chukulia mfano unamfumania mkeo, au unakuta analijamaa wanabusiana etc, au unajikuta mkeo amekuandika kwenye hirizi aliyoficha chumbani kwako anataka kukuua ili achukua mali ulizochuma kwasababu wewe umemuoa yeye juzijuzi tu hapa...kuna mambo mengi sana yanaweza kumprovoke mtu akajikuta amempiga mwanamke pasipo akili yake, ndo inayoitwa provocation, unapokuja kustuka kuwa unampiga mtu, umeshamaliza kazi. THATS WHY NIMESEMA INATEGEMEANA.
pia, inategemeana na watu hao kama wameokoka na Mungu anawasaidia kuwashindia dhambi au la. Mtu kama hajaokoka, kuna siku tu atapiga mkewe, na wewe mke kama jamaa lako halijaokoka, kuna siku litakutandika tu, its just a matter of time. WHY, ni kwasababu roho ya ukatili ya makata inaweza kumwingia mtu yeyote ambaye hajaokoka popote pale, na ulizi pekee ni kuokoka uli Damu ya Yesu iwe ndani yako mapepo yasikuingie...ukiwa haujaokoka, lolote laweza kutokea...pia, nyie mnaochukua vimada, hivyo vinyumba vidogo huwa vinaweka dawa toka kwa waganga ya kuwagombanisha ninyi na wake zenu, utamtandika mkeo bila hata kujijua, siku unapokuja kustuka madawa yakiisha nguvu, ameshakuchuna, kahamia kwa bwana mwingine, na wewe umepoteza watoto na mkeo wa ndoa au watoto wanahangaika kwa kwashakoo uliwatelekeza na kimada kakomba hela zote umefukuzwa kazi mifuko yote nje....macho pafupafupafuuuu.
kuna sababu nyingi zinazofanya wanandoa kupigana, ndo maana nasema inategemeana, narudia tena inategemeana.
nilipokuwa duniani huko misri, nilimtwanga sana mke wangu, na ikichukulia mimi nilikuwa na black belt ya karate, lakini nilipookoka, ile roho iliondoka na sijui ilienda wapi, sasaivi nachukia kupigana, hata kwenye tv nikiona watu wanapigana either boxing au karate hata mikanda ya action huwa naondoka sipendi hata kuangalia, Yesu huyo anafnaya mabadiliko ndani ya mtu. ndoa yangu ina upendo kama wakati ule tulipokuwa wachumba wabichi..yaani upendo ule mtamuuuuu, na wengi huwa wanatushangaa tunapoitana honey na darling hadi leo baada ya miaka mingi ya ndoa yetu..NASUBIRIA VIRUNGU TOKA KWENU NAJUA WENGI MTANITANDIKA KWA KAULI HII, LAKINI UKWELI NDO HUO~