Mwanaume unawezaje kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili?

Mwanaume unawezaje kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili?

Kaunara

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
249
Reaction score
452
SIjui mila desturi na taratibu za makabila mengine. Ila ukweli hata kama umeoa kwenye familia ya kitajiri kwenda kukaa ukweni zaidi ya wiki mbili aisee unajidhalilisha.

Mzee wangu aliniambia ukikaa ukweni siku mbili zinataosha sana ya tatu unaondoka hii ni kwamba usijue maisha yao na wao wasijue mipango yako. Ukikaa sana ukweni kuna siku utatumwa chumvi dukani uone wanakudharau kumbe mipango yako sio.

Chini ya hili jua kuna wanaume achilia mbali kwenda kusalimia ukweni, wapo ambao wanaishi ukweni. Na hapo mtu anahitaji haishimike. Aisee ukiona unaishi ukweni na mwanamke anakuheshimu wee jamaa hata mbingu ni yako. Nawasilisha.
 
Nawakilisha

Hilo neno la mwisho linaharibu utamu wa maudhui uliyotoa hapo juu yaani hapo umeonesha ww ni mwakilishi wa hao wanaokaa ukweni.

Back to the point kwakweli binafsi ukweni labda uwe ni msiba mzito ndo unaweza kuniweka siku3 kinyume cha hapo ni siku mbili au moja nasepa tena nitarudi huko baada ya muda mrefu kupita kama hakuna shida yoyote
 
Hilo neno la mwisho linaharibu utamu wa maudhui uliyotoa hapo juu yaani hapo umeonesha ww ni mwakilishi wa hao wanaokaa ukweni.

Back to the point kwakweli binafsi ukweni labda uwe ni msiba mzito ndo unaweza kuniweka siku3 kinyume cha hapo ni siku mbili au moja nasepa tena nitarudi huko baada ya muda mrefu kupita kama hakuna shida yoyote.
Nawakilisha ni tofauti na nawawakilisha
 
Back
Top Bottom