Mwanaume usiishi kwa kutegemea eti kuna watu mbele watakusaidia

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
LEO TUONGEE NA WANAUME ✍️

Mijini hasa majiji haya makubwa kama Dar unaweza kutana na mwanaume akakuomba shilingi mia tu ya muhogo ila kila ukimwangalia unabaki na maswali mengi, sio vibaya kuomba ila nani anafanya hivyo? Na ukiangalia yuko tu kijiweni na hana ulemavu.

Mara kadhaa unaweza sikia vijana wa kiume wanajinadi kuwa wao hawatafuti sana kwa sababu wana watu mbele, sio mbaya kusaidiana ila kijana wa kiume unaishije kwa kutegemea walioko mbele?

Mara kadhaa unaweza sikia vijana wa kiume kutwa kulalamika kuwa maisha yao ni magumu kwa sababu hawana ndugu mbele wa kuwasaidia, kweli kijana wa kiume unaweza ishi kwa kutegemea ndugu wakusaidie?

UKIZALIWA WA KIUME JUA WEWE NDIO UNATAKIWA UWE MBELE UJISAIDIE NA KUSAIDIA UKOO WAKO.

Kama unalalamika huna mtu mbele wa kukusaidia basi wewe jua ni makosa yako kwa sababu wewe ndio unatakiwa uwe mbele sasa utafikaje hiyo ndio maana halisi ya kuwa MWANAUME ni lazima upambane kwa sababu uwezekano wa mwanaume kuonewa huruma ni mdogo sana hivyo bila juhudi zako utasubiri sana.

Barabarani mwanamke akionekana analia watu watajua tu kuna tatizo na wataonyesha nia ya kumsaidia ila wewe wa KIUME ukionekana unalia barabarani kwa haraka utaonekana KITUKO na wataenda mbali zaidi watajua ni BANGI zimekukataa 😔

Inamaanisha nini? WANAUME tuna machaguo mawili tu makubwa ambayo ni;

1.Tupambene tuwe mbele KUJISAIDIA

2.Tulegee ila tukubali KUISHI KWA KULALAMIKA MUDA WOTE KUWA KUNA WATU WALIPASWA KUTUSAIDIA ILA WAMEGOMA.

Mwanasayansi Saul kalivubha.
#fikia ndoto zako
 
Si mateso excactly but jamii ni high expectation kwa mwanaume kokote alipo, wana expect a leader, provider, msuluishi. Is why atabeba kila kitu, thats where so called mateso comes from
Hii ni kweli, mwanaume huangaliwa kama vile hakuna kinachomshinda
 
Mateso ni...kuzaliwa mwanaume moja, mbili kuzaliwa afrika hasa tz..........
Una kitu, sema heri mara 10 tz sio kuzaliwa Congo, Sudan vita mwanzo mwisho.. Chad kwenye maukame huko tuna afadhali asee

Bongo na Haiti bora Tz
 
LEO TUONGEE NA WANAUME ✍️

Mijini hasa majiji haya makubwa kama Dar unaweza kutana na mwanaume akakuomba shilingi mia tu ya muhogo ila kila ukimwangalia unabaki na maswali mengi, sio vibaya kuomba ila nani anafanya hivyo? Na ukiangalia yuko tu kijiweni na hana ulemavu.

Mara kadhaa unaweza sikia vijana wa kiume wanajinadi kuwa wao hawatafuti sana kwa sababu wana watu mbele, sio mbaya kusaidiana ila kijana wa kiume unaishije kwa kutegemea walioko mbele?

Mara kadhaa unaweza sikia vijana wa kiume kutwa kulalamika kuwa maisha yao ni magumu kwa sababu hawana ndugu mbele wa kuwasaidia, kweli kijana wa kiume unaweza ishi kwa kutegemea ndugu wakusaidie?

UKIZALIWA WA KIUME JUA WEWE NDIO UNATAKIWA UWE MBELE UJISAIDIE NA KUSAIDIA UKOO WAKO.

Kama unalalamika huna mtu mbele wa kukusaidia basi wewe jua ni makosa yako kwa sababu wewe ndio unatakiwa uwe mbele sasa utafikaje hiyo ndio maana halisi ya kuwa MWANAUME ni lazima upambane kwa sababu uwezekano wa mwanaume kuonewa huruma ni mdogo sana hivyo bila juhudi zako utasubiri sana.

Barabarani mwanamke akionekana analia watu watajua tu kuna tatizo na wataonyesha nia ya kumsaidia ila wewe wa KIUME ukionekana unalia barabarani kwa haraka utaonekana KITUKO na wataenda mbali zaidi watajua ni BANGI zimekukataa 😔

Inamaanisha nini? WANAUME tuna machaguo mawili tu makubwa ambayo ni;

1.Tupambene tuwe mbele KUJISAIDIA

2.Tulegee ila tukubali KUISHI KWA KULALAMIKA MUDA WOTE KUWA KUNA WATU WALIPASWA KUTUSAIDIA ILA WAMEGOMA.

Mwanasayansi Saul kalivubha.
#fikia ndoto zako
Hii tunaaiita alpha thread..
 
Back
Top Bottom