Mwanaume usimuanike mpenzi wako mitandaoni

πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Mimi ambao hawaposti ninawaona wanahoja ikiwa ni maamuzi na hawapendi kufanya hivyo lakini hawa wanaoogopa kuachwa au kuchapiwa naona ndio wanamatatizo makubwa
Hao ni waoga kwani waliambiwa hii dunia wanaishi malaika..?? Wao wapost wakiachana basi ni sehemu ya maisha, watafute wengine wawapost kazi iendelee..!!
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Mimi ambao hawaposti ninawaona wanahoja ikiwa ni maamuzi na hawapendi kufanya hivyo lakini hawa wanaoogopa kuachwa au kuchapiwa naona ndio wanamatatizo makubwa
swala sio kupenda au kujali hiyo ni dosari ya uelewa na Ufahamu juu ya mahusianao, uchumba na ndoa πŸ’

wenye Ufahamu na uelewa wa kutosha, hiyo haiwezi kua hoja kwenye mapenzi yao unless wamekutanishwa na mtandao πŸ’

R I P Laigwanan comrade ENL
 
Aende Mahakamani akaangalie idadi ya talaka alafu hao wanaopeana talaka kwa ugoni ahesabu wangapi waliwahi kuwapost wenza wao.
Wewe ndio ulitakiwa ulete hizo takwimu sasa za walioenda mahakamani ila kumpost mpenzi kwenye mitandao ya kijamii ni ushamba lini GSM MO DEWJI BAKHRESA amepost mke wake kwenye social platforms lete hapa wake tuwaone kama ww una kawaida ya kupost mpenzi wako basi tambua huo ni ushamba hakuna tajiri duniani ana huo mda au mtu anayejielewa anafanya huo upuuzi.
 
swala sio kupenda au kujali hiyo ni dosari ya uelewa na Ufahamu juu ya mahusianao, uchumba na ndoa πŸ’

wenye Ufahamu na uelewa wa kutosha, hiyo haiwezi kua hoja kwenye mapenzi yao unless wamekutanishwa na mtandao πŸ’

R I P Laigwanan comrade ENL

Mkuu kwa uelewa wako mtandaoni Watu wanatakiwa wapost jambo gani?
 
Sianzi na salamu kwasababu hata nikiwasalimia hamuitikii anyway let's go stright to our topic.

Unajua vijana wa siku hizi na baadhi ya watu wamekuwa wajinga sana ila wao wenyewe wanajiona wajanja na hata ukiwashauri wanakuona mshamba. Kumpenda mke wako au mpenzi wako sio lazima mpaka umpost mitandaoni kwasababu maisha ya mitandaoni na uhalisia ni tofauti watu wengi wanachokipost sicho wanachokiishi mimi leo kazi yangu kuwakumbusha tu.

Wakati tunaelekea kwenye valentine's day epuka huo mkenge mapenzi yalikuwepo kabla ya Instagram Facebook na WhatsApp jitambue epuka stress ambazo hazina msingi na zina epukika.

Sasa kabla hatujafika mbali ngoja nikupe mifano ya watu ambao mapenzi yamewatokea puani baada ya kuanikana mitandaoni na kujifanya wao kina sharkan na kajol.

NICK WA PILI NA MKE WAKE: Hawa bwana walifanya watu wengine wote waonekane wajinga kwasababu jinsi walivyokuwa wakiishi mitandaoni mpaka kufikia hatua ya mwanaume kusema hata akipewa nafasi ya kuoa tena atamuoa mke wake kwa mara ya pili ila mwisho wa siku shetani akaingia kati kilichotokea kila mtu alikiona. Watu walienda kula nyama nje ya nchi na ndio ikawa mwanzo wa matatizo yao.

DR. DR. MWAKA NA MKE WAKE: Hawa walifika mpaka hatua ya kufanya interview na kusema analala na wake zake kitanda kimoja na alikuwa mshauri mkubwa wa mahusiano kabla hayajamkuta, ila anachopitia sasa hivi ni maumivu mpaka kaamua kufunga comment section kwenye mitandao ya kijamii sasa fikiria muuza dawa za nguvu za kiume na mshauri wa ndoa anateseka demu anakula maisha na wanyamwezi wengine huko sasa mateso yote ya nini mzigo wahuni wanakula huko.

MANARA NA WAKE ZAKE WAWILI: Huyu jamaa anajifanya much know yaani yeye anajiona mjanja kuliko watu wote na kila kitu anajua yeye hata baada ya mzee Yusuph kumshauri alimjibu jeuri kama kawaida yake ila mwisho wa siku ndoa chalii licha ya kuwapeleka Dubai na Qatar lakini ngoma ilikuwa ngumu mwisho wa anayeteseka ni yeye ila anajikaza kwasababu yule jamaa hakubali kushindwa. Mizigo watu wamechukua huko safari za Dubai haziishi mapemzi haya.

MC PILIPILI NA MKEWE:Yaani katika watu waliotakiwa watulie ni hyo MC kwasababu kwa waliosoma UDOM na maisha aliyokuwa anaishi mke wake chuo alikuwa mdangaji pro max ila kwasababu MC ni mshamba akaona kapata mke akaweka ndani anayopitia sasa hivi anajua mwenyewe maumivu yake sasa kwa nini uteseke wakati mateso yana epukika. Mdangaji hawezi kusahau kazi yake angetulia kupunguza maumivu.

MADEBE NA MKEWE: Huyu jamaa alikuwa anajifanya mshauri wa masuala ya ndoa ila ni wahuni kama wahuni wengine baada ya mke wake kuelezea aliyokuwa anamfanyia wakiwa kwenye ndoa na kinachoendelea sasa hivi ni aibu kwa wote wawili kwasababu kila mmoja hakubali kushindwa. Ila kama sio mitandaoni kuanikana hzi taarifa walitakiwa wamalizane wenyewe tu ila kwasababu washazoea mitandao ilikuwa haliepukiki.

STAMINA NA MKEWE: Katika watu waliopitia kipindi kigumu kwenye ndoa na mapenzi ni huyo jamaa maana alifikia hatua mpaka ya kutaka kujiua baada ya ndoa yake kufika tamati na kupelekana mahakamani mpaka leo habari za ndoa na wanawake hataki kuzisikia na amejifunza kuto anika mademu hovyo hovyo maana ilikuwa tunamkosa kama sio watu kuingilia kati.

DULA MAKABILA NA ZAYLISA: Wasanii wetu wana heka heka nyingi sana yaani wanaishi maisha ya kuigiza mpaka kwenye ndoa mwisho wa siku wanabaki kuaibika na kudhalilika alichokuwa anakifanya makabila na mkewe ni kama vile watu wote walikosea kuoa yeye peke yake ndio ana mke mzuri na ndio wanapendana kuliko watu wote duniani. Ila amepata funzo kwasababu kilichomkuta kila mtu anakijua.

RICARDO MOMO NA MKEWE: We jamaa mshamba mshamba unapata bahati ya kuwa na pisi kali kama ile halafu una iyanika mara kwa mara unapost mitandaoni wahuni wamepita naye amebaki kulia tu demu haipiti week kaenda Dubai mateso yote ya nini fanya mambo kimya kimya kuepuka maumivu kwasababu yana epukika. Mitandao sio mizuri kwa wanandoa na wapenzi nikujitia stress tu.

NB:KUPOSTIANA MITANDAONI SIO ISHARA YA UPENDO NI KUTAKA KUKOMOANA AU KUJIONYESHA TU KWA WATU ILA NI TOFAUTI NA UHALISIA.
Mbona mke wa ricardo momo anaonekana wakupigwa na kuacha yeye ndo kaoa kabisa
 
[emoji2][emoji2][emoji2]
Mimi ambao hawaposti ninawaona wanahoja ikiwa ni maamuzi na hawapendi kufanya hivyo lakini hawa wanaoogopa kuachwa au kuchapiwa naona ndio wanamatatizo makubwa
Yaani ww inaonekana ni wale watu wakiweka WhatsApp status inakuwa kama tairi yaani status 50 kwa siku huo si uwendawazimu halafu hamna cha maana hata kimoja.
 
Mke ni pambo la ndani ya nyumba unampost mitandaoni ili umringishie nani? Kama sio kuwapa tamaa watu waanze kupanga mipango ya kishetani
 
Ndio ileile concept kuwa Mwanamke WA Ofisini anazagamuliwa huko ofisini hivyo wanaume waoe golikipa.
Yaani kuna Watu wanafikiri kwa namna ya ajabu sana
Ni kweli wala sio uongo japo suingi mkono kuoa goli kipa nishawahi kuhudhuria semina moja tulikaa week yaliyokuwa yakiendelea mungu ndio anajua wanawake wanapenda mserereko sana hudhuria siku moja halafu uje na andiko ww si mtaalam wa fasihi.
 
Wewe ndio ulitakiwa ulete hizo takwimu sasa za walioenda mahakamani ila kumpost mpenzi kwenye mitandao ya kijamii ni ushamba lini GSM MO DEWJI BAKHRESA amepost mke wake kwenye social platforms lete hapa wake tuwaone kama ww una kawaida ya kupost mpenzi wako basi tambua huo ni ushamba hakuna tajiri duniani ana huo mda au mtu anayejielewa anafanya huo upuuzi.

Anhaa! Kumbe wewe unamuiga GSM, MO Dewji na kina Bakhressa.
Sasa ndugu yangu wewe hata milioni moja kwenye akaunti huna alafu unafikiri kina MO NI mabilionea kwa sababu hawaposti Wake zao.

Kwenye akaunti za hao uliowataja wanapostigi nini kama unawafuatilia?
 
Ni kweli wala sio uongo japo suingi mkono kuoa goli kipa nishawahi kuhudhuria semina moja tulikaa week yaliyokuwa yakiendelea mungu ndio anajua wanawake wanapenda mserereko sana hudhuria siku moja halafu uje na andiko ww si mtaalam wa fasihi.

Wakati unaenda kazini unamuacha mkeo nyumbani unajua huku nyumbani anafanya nini?

Kama unaelimu walau ya kidato cha nne huwezi kuwaza kwa namna uliyowaza.
 
Anhaa! Kumbe wewe unamuiga GSM, MO Dewji na kina Bakhressa.
Sasa ndugu yangu wewe hata milioni moja kwenye akaunti huna alafu unafikiri kina MO NI mabilionea kwa sababu hawaposti Wake zao.

Kwenye akaunti za hao uliowataja wanapostigi nini kama unawafuatilia?
Ndio ujue wewe kama unafanya hivyo hujielewi hao ndio successful people in our country sasa kwa nini wasiwe role model kwa hyo ww million 10 kwako ndio kipimo cha utajiri ndio nyie mnakopa million 10 bank mnakatwa miaka nane kwa ideology hizo mimi ukiniletea hapa watu wanaojielewa kama hao tutaenda sawa sio unapost 24/7 na status zinakuwa kama tairi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] leo ndio nimejua wewe ni mtu wa aina gani.
 
Yaani ww inaonekana ni wale watu wakiweka WhatsApp status inakuwa kama tairi yaani status 50 kwa siku huo si uwendawazimu halafu hamna cha maana hata kimoja.

Kwenye uhalisia.
Wewe na Nick WA pili, Haji Manara na hao uliowataja kuna yeyote kwenye ukoo wenu anatija kuwashinda hao ndani ya taifa licha ya kuwa hampost Wake na wenza wenu?

Unachoshindwa kuelewa ni kuwa, jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi au sheria za Mungu sio kosa kufanya. Na ukiona unamkamnya mtu asifanye jambi ambalo sio kosa ujue wewe ndio unamatatizo Makubwa
 
Kila uhusiano unaudhaifu wake kwahiyo kuna watu kazi yao ni kusoma udhaifu huo, kwahiyo ukilega kidogo tu watu wanapita nae pia msisahau kuwa pesa ndio jibu la mambo yote
 
Back
Top Bottom