Watu8
Platinum Member
- Feb 19, 2010
- 73,773
- 102,126
Katika ugunduzi wa kushangaza, mgonjwa wa kiume mwenye umri wa miaka 66 huko Hong Kong alijikuta akiambiwa na madaktari kuwa yeye ni mwanamke pindi alipokwenda hospitalini kwa ajili ya kutafuta matibabu ya uvimbe tumboni.
Madaktari wamegundua kwamba uvimbe huo ni matokeo ya uzibaji wa vifuko "cyst" kwenye ovari yake na kwa mantiki hiyo mwanaume huyo alikuwa ni mwanamke.
Tukio hili liliripotiwa na madaktari kutoka hospitali ya Kwong Wah na ile ya Malkia Elizabeth, ambapo mgonjwa huyo alikuwa akitibiwa.
"Kwa ufafanuzi, mgonjwa ni mwanamke ambaye hawezi kupata mimba. Lakini pia ana vichocheo vya adrenal hyperplasia (CAH), ambavyo vinampa muonekano wa mtu mume (mwanaume)," alisema Profesa Ellis Mhe Kam-Lun wa Chuo Kikuu cha Zhonguo Daxue.
"Ni jambo la kuvutia na ni nadra sana ya kuwa na mchanganyiko wa jinsia mbili. Pengine kuna uwezekano tukio kama hili kutoonekana tena katika siku za usoni", aliongeza.
Kwa maelezo zaidi fuatilia hapa chini...
Mwanaume wa Kichina agundulika kuwa ni Mwanamke...