Mwanaume wa Kichina agundulika kuwa ni Mwanamke...

Mwanaume wa Kichina agundulika kuwa ni Mwanamke...

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
73,773
Reaction score
102,126
M_Id_390828_Chinese_Man_.jpg

Katika ugunduzi wa kushangaza, mgonjwa wa kiume mwenye umri wa miaka 66 huko Hong Kong alijikuta akiambiwa na madaktari kuwa yeye ni mwanamke pindi alipokwenda hospitalini kwa ajili ya kutafuta matibabu ya uvimbe tumboni.

Madaktari wamegundua kwamba uvimbe huo ni matokeo ya uzibaji wa vifuko "cyst" kwenye ovari yake na kwa mantiki hiyo mwanaume huyo alikuwa ni mwanamke.

Tukio hili liliripotiwa na madaktari kutoka hospitali ya Kwong Wah na ile ya Malkia Elizabeth, ambapo mgonjwa huyo alikuwa akitibiwa.

"Kwa ufafanuzi, mgonjwa ni mwanamke ambaye hawezi kupata mimba. Lakini pia ana vichocheo vya adrenal hyperplasia (CAH), ambavyo vinampa muonekano wa mtu mume (mwanaume)," alisema Profesa Ellis Mhe Kam-Lun wa Chuo Kikuu cha Zhonguo Daxue.

"Ni jambo la kuvutia na ni nadra sana ya kuwa na mchanganyiko wa jinsia mbili. Pengine kuna uwezekano tukio kama hili kutoonekana tena katika siku za usoni", aliongeza.

Kwa maelezo zaidi fuatilia hapa chini...

Mwanaume wa Kichina agundulika kuwa ni Mwanamke...
 
Ukisema mwanamme wa kichina, inakuwa kichina china tu.

Dah, ndio unakuta kama kaona labda hapati watoto
Kwa enzi zetu za zamani mwanamke aliyeolewa ananyanyaswa hazai, anamaliza chakula bure, kumbe mmewe mwanamke.
This world will never be fair kabisa.
 
Sipati picha baada ya kupewa hayo majibu kua yeye ni ke...saikolojia yake inasoma kichinachina tu
 
Nilitamani nimuone akiwa amebeba ujauzito wake ili nijue angeonekanaje.
 
dunia ina mambo..........sasa siku zote alikuwa vipi?
 
Sipati picha baada ya kupewa hayo majibu kua yeye ni ke...saikolojia yake inasoma kichinachina tu

Sidhani kama alishtuka maana miaka yote amekuwa akijijua kuwa yeye ni ME na baada ya hiyo operesheni bado kaendelea kuishi kama ME....
 
mwanaume amegudulika kuwa mwanamke, loh sasa yeye sio mwanaume, je chini ana mkia au kitobo?
 
Kama anajijua yeye ni mwanaume bila shaka hana kitobo

mwanaume amegudulika kuwa mwanamke, loh sasa yeye sio mwanaume, je chini ana mkia au kitobo?
 
dunia ina mambo..........sasa siku zote alikuwa vipi?

Alikuwa anaishi tu kama mwanaume...assume hivi, siku moja uhisi una maumivu maneno ya kinena...unaamua kwenda hospitali kupima...majibu yanatoka kuwa una korodani ambazo zipo ndani na ndizo zimepata uvimbe.
Case kama hiyo ndiyo iliyompata huyu kizee
 
hivi mtu anaitwa mwanaume au mwanamke kwa kutegemea nini hasa? je kuna jambo jengine zaidi ya kitobo na mkia?
 
Alikuwa anaishi tu kama mwanaume...assume hivi, siku moja uhisi una maumivu maneno ya kinena...unaamua kwenda hospitali kupima...majibu yanatoka kuwa una korodani ambazo zipo ndani na ndizo zimepata uvimbe.
Case kama hiyo ndiyo iliyompata huyu kizee

ni ngumu kumeza lakini ningekubali tu matokeo!!!
 
Back
Top Bottom