Mwanaume wa kweli, na ukweli juu ya kuyaishi maumivu

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,951
Reaction score
19,766
Salaam jamiiforum.

Mwanaume unataka raha?

Mwanaume unadeka?

Mwanaume unasound kike kabisa,na ukipewa zawadi unalia,yaani kuna mshipa wa hisia unaokuteka na kuuharibu uanaume wako?

Hii si sawa,Leo ni siku ya mwisho wa Mwezi wa tatu mwaka 2026.
Karne ya 21 uliyobeba taswira nyingine ya wanaume ambayo awali haikuzoeleka.

1.Wanaume kupenda kulelewa.

Jamani hapa tunapoteza mabingwa wengi na kupoteza nguvukazi yaani mwanaume 35+ unawaza kabisa kutoboa kimaisha kupitia mwanamke, ambaye si dada yako,mama au Shangazi,ni mtu ambaye akiamua kukudumb ni suala la muda tu,au akipata handsome kukuzidi na anayeiweza kazi basi umeachwa.
Shituka.

2.Wanaume kukwepa majukumu.

Sasa hivi ukipita kwenye vijiwe vingi,na maeneo mengi utagundua namna wanaume walivyo dhaifu,hawahongi,hawahudumii wapenzi wao Kwa kigezo cha kuona wanawake wanapenda pesa sasa wewe nafasi yako ni ipi.

Oyaaa sanuka, wanawake wazuri wapo tena wenye mapenzi ya dhati,jukumu la ulinzi,huduma na kumcare Kwa lolote ni lazima na siyo kukimbia majukumu,nyie ndo mnasababisha mahusiano au ndoa nyingi kuvunjika kwasababu hamuwaoneshi wapenzi wenu Nia,kusudi na hatma ya mahusiano yenu mwisho wa siku mnakimbiwa,huku mkisingizia mmepiga chini.

3.Kupenda anasa zisizoendana na kipato chako.

Bro to bro,

Pombe haipo Kwa ajili ya mtu masikini au anayejitafuta,badala yake ni watu watatu wanaruhusiwa
1️⃣ Mtu mwenye uwekezaji mkubwa.
2️⃣Mstaafu anayetumia pensheni.
3️⃣Born town,dili chafu, illegal missions,yaani asubuhi hana kitu saa kumi jioni ana milion 50 ni zake hajakopa Kwa mtu.siyo wewe saidia fundi mwenye chumba kimoja huku ukilaza wakwe Kwa majirani

4.Fanya kazi Kwa bidii.

Maisha mazuri si kusoma sana,Bali ni namna unavyowaza na kufikiri vizuri.

Ni miezi miwili nimetembea mikoani nikitafuta mizigo yangu fulani,nikagundua namna watu wanavyoumia huku wakifaidi maumivu na muda waliowekeza

Kijana wa miaka 35 hadi 40,ana trekta tatu ,fuso mbili,yaani anavyoijadili milioni Mia nikama anaigiza lakini kumbe anayo kweli na kijana huyu haijui dar kila kitu anaagiza analetewa.

Mtoto mdogo anamiliki mashamba

Makubwa ya mpunga,mahindi huku akiheshimika kwani ana ndoa imara watoto wa kutosha,mtu huyu hajamaliza hata darasa la saba ana semi huku ikipiga mishe za kutosha ,cha ajabu Dar es salaam unaijua wewe yeye hana haja kupajua

Lakini vijana wengi wapo mjini hapa kazi kujisifia ujinga ,unafanya kazi isiyoeleweka huku ukiwa unahudhuria viwanja vya gharama ,kifuatacho unaanza kujichekesha mbele ya wanaume wenzio eti unataka kampani, kwenye bill ikimiss 20k huna cha kuchangia,sasa starehe za nini?

5.@jack Daniel ni jitu la kijijini tena shamba limekuja mjini ili lisaidiwe kielimu walau kutengeneza Kesho iliyo Bora,ni tall and handsome.
Halijisifii ni kwamba linaambiwa hivyo miaka mingi.
But halijawahi kulelewa licha ya kupata usumbufu sehemu tofauti tofauti.

Niliwahi kupitia msoto haswa ila sijawahi kutamani maisha yasiyo yangu.

Niliwahi kuambiwa nitakatiwa ticket ya ndege niende ng'ambo nikajiliwaze lakini sikufanya hivyo,niliona ni ujinga badala yake nikaingia kijiweni nikapewa canter tani tatu nikawa napiga mishe kama kawaida,kutoka kwenye mega office,kujidai salary nzuri hadi deiwaka.yote hayo ni kawaida Mwanaume lazima upambane huku ukikubali mabadiliko hata Nyakati zikiwa mbaya.

Acheni ujinga wazee.

Mabroo mnazingua.

Hii ni Tuesday kwangu ni kama weekend tu ni mwendo wa castle lite tangu ijumaa.

Karibuni
 
N kwel kaka ,mwanaume afai kuwa tegemez.Ajipambanie maana mafanikio haiji kwa mkato,ila n kupamban na kutokataa tamaa.Ila mwanangu nimekubali kinom,maana ww n faita asante kwa ushaur
 
Uzi wote umelala hapa, hayo mengine porojo tu
 
Naona unawasimanga Vijana wenzio

Ila kimsingi haipendezi Mwanaume 35+ awe na hizo tabia ulizoandika, ndiyo mwanzo wa kupoteza Ubingwa Vijana wanasemaga 😂🙌

Kwasisi age go hatuna cha kuchangia, kwasababu ulabu tunapiga, pia tunavuta Kiko zetu kwa hela zetu za pension, maana kama kusomesha tulishamaliza tangu mwaka 47 😜
 
Yote uliyosema nakubaliana na wewe ila issue ya kusema eti ukimuhudumia mke ndio ndoa itakaa sawa au Mwanamke wako hatakuacha,hapo bado hujawajua wanawake vizuri mkuu,

Wanawake wenyewe hua hawajui wanataka nini.
 
Naona unawasimanga Vijana wenzio
Amewasimanga vijana wa Daslam,
Ni kweli kwa sisi wakubwa tunakula tu maisha,enzi zetu hakukua na haya mambo ya mwanaume kulelewa na mshangazi.
 
Amewasimanga vijana wa Daslam,

Ni kweli kwa sisi wakubwa tunqkula tu maisha,enzi zetu hakukua na haya mambo ya mwanaume kulelewa na mshamgazi.
Hahaha.....amewapiga nondo za kutosha 😂

Najua lazima watakuja na comeback heavy 😜

Sisi age go tulishaweka mitikasi ya kutengeneza maokoto daily

Kwahiyo hata tukishinda weekend Viwanja tunakula monde inakuwa monile hadi naiti 😎
 
Huu uzi utageuka kua uwanja wa vita soon.
😀😀
 
Kama ilivyo mwanamke akiwa karibu sana na wanaume anakuwa na vitabia vya kike ndo hivyo hivyo mwanaume
 
Vijana wenzangu?

Umeambiwa Mimi ni kijana?

55+plus
 
N kwel kaka ,mwanaume afai kuwa tegemez.Ajipambanie maana mafanikio haiji kwa mkato,ila n kupamban na kutokataa tamaa.Ila mwanangu nimekubali kinom,maana ww n faita asante kwa ushaur
Yes kama kawaida yetu
 
Dah engineer ,umegonga nondo haswa .
 
Wanaume wa dar es saalam mumesikia hayo,mm nkiw mmoja wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…