mwanaume.

mwanaume.

Lady G

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2010
Posts
515
Reaction score
131
heshima kwenu wakuu.

Naomba kuelimishwa juu ya tohara kwa wanaume.

1. Kuna athari gani ya kwa mwanaume kutotahiriwa
2. Madhara gani atapata mwanamke kwa kufanya mapenzi na un sakamsaizd man
3. Mwanaume akiwa mtu mzima anaweza kufanyiwa tohara
4. Kuhusu utamu unakua ulele ka iliyomenywa? Thanx wakuu.
 
Madhara ya kutotahiriwa ni kupata magongwa ya kuambukizwa kwa urahisi kwa mujibu wa madaktari. Ndiyo maana wanashauri wanaume kutahiriwa ili kupunguza maambulizi ya ukimwi. Mengine watajibu wenye utaalam zaidi. Ila hata watu wazima wanaruhusiwa kutahiriwa sijasikia kama kuna matatizo yoyote labda aibu tu.
 
Asante sana mkuu kwa maelezo yako, nina ndugu yangu tunahitaji kumsaidia juu ya hili. Gal friend wake amekuja kuomba ushauri na mie sikuwa na ufahamu wowote. Asante sn
 
heshima kwenu wakuu.

Naomba kuelimishwa juu ya tohara kwa wanaume.

1. Kuna athari gani ya kwa mwanaume kutotahiriwa
2. Madhara gani atapata mwanamke kwa kufanya mapenzi na un sakamsaizd man
3. Mwanaume akiwa mtu mzima anaweza kufanyiwa tohara
4. Kuhusu utamu unakua ulele ka iliyomenywa? Thanx wakuu.

Majibu:

1. Hakuna madhara ya kutahiriwa kama tohara itafanyika na daktari au ngariba mzuri. Uzuri wa tohara ni kuwa mwanaume anaweza kujiweka katika hali ya usafi kirahisi na kupunguza infection. Kichanga kufanyiwa tohara saa nyingine kunaweza kuuharibu uume wake kwa sababu bado mdogo na daktari anaweza kukata pasipo lakini huwa anapona haraka kuliko mtu mzima. Kufanyiwa tohara kienyeji (jando) kunaweza kuwa na athari zake. Naomba uangalie hii documentary (NOT X-rated) toka South Africa.

Ndiyindoda: I am a man - People & Power - Al Jazeera English

2. Hakuna madhara makubwa kwa mwanamke akifanya mapenzi na mume asietahiriwa hasa kama wako kwenye monogomous relationship. Kama mume ana wanawake wengi basi inakuwa rahisi kwake kusambaza magonjwa (kama yeast infection, nk.) kutoka mmoja hadi mwengine.

3. Ndio, mtu mzima anaweza kufanyiwa tohara. Baada ya kidonda kupona anaweza kuwa na sensitivity kidogo wakati wa kufanya mapenzi lakini hiyo itapita haraka sana. He will be back in full swing before he knows it.

4. Kwa mwanamke hataona tofauti yoyote katika utamu pre and post tohara ya mpenzi wake. Kwa mwanamme pia utamu utabaki palepale bali zingatia jibu na. 3.

I hope this helps.
 
Tohara (kutoka Kiarabu طهارة tahara - safi, tahiri) ni upasuajimdogo wa kukata na kuondoa govi, yaani ngoziinayofunika kichwa chauume.
Wakati mwingineukeketaji huitwa "tohara ya mwanamke".
Inaweza kufanyika katika umri wowote na kwa sababu za kiutamaduni, za kidini au za kiganga. Mara nyingi desturi za kutahiri

zinachanganya sababu za kidini na kiutamaduni. Kwa mfano, Waislamu wa
Misri huamini ya kwamba wanatahiri watoto wao kama amri ya kidini lakini Wakristo Wakopti wa nchi hiyo hutahiri watoto vilevile. Ukweli ni kwamba tohara inajulikana ilikuwa

desturi ya Wamisri tangu kale.
Tohara inafanyika hasa mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto au wakati wa kubalehe.
Kufuatana na Shirika la Afya Duniani takriban 30% za wanaume wote duniani wametahiriwa, wengi wao wakiwa Waislamu.

Tohara ya kiutamaduni

Katika
makabilamengi ya Afrikamvulana anatahiriwa ili kuingizwa katika kundi la wanaume wanaopaswa kuwajibika katika jamii.
Desturi hiyohiyo inaonekana pia kati ya watu wa
Pasifikik.mf. Wapolinesia wa Samoa, Tonga na Niue, vilevile kati ya

Wamelanesia wa
Fiji na Vanuatu.
Wakazi asilia wa Australia huwa pia na tohara ya wavulana.

Tohara kama amri ya kidini

Uyahudi

Kwa
Wayahudi tohara ni ishara ya agano lao na Mungu na inapaswa kufanyika siku ya nane baada ya mtoto wa kiume kuzaliwa ili kumwingiza mapema katikataifa la Mungu.
Kufuatana na habari za
BibliaIbrahimu alikuwa mtu wa kwanza aliyepokea amri ya kutahiriwa kama alama ya agano (Mwanzo 17).

Ukristo

Yesu mwenyewe alitahiriwa siku ya nane kama Wayahudi wote wa kiume. Tohara ya Yesu inakumbukwa kwa sikukuu maalumu katika makanisa mengi duniani hasaWaorthodoksi.

Agano Jipya inaonyesha jinsi gani suala la tohara lilikuwa motomoto mwanzoni mwa
Kanisa, wakati Wakristo wengi walitoka katika Uyahudi.

Kufuatana na kitabu cha
Matendo ya Mitume (15:23-29) Mtaguso wa Mitume uliofanyika Yerusalemu uliamua Wakristo kutoka mataifa wasilazimishwe kutahiriwa.

Hasa
Mtume Paulo alisisitiza kwamba jambo hilo si muhimu tena, cha maana ni kuwa watu wapya kwa imani.
"Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya"
(Gal 6:15).
"Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili"
(Fil 3:3).
Hata hivyo Wakopti wa Misri na
Ethiopia wameendelea kutahiri watoto wao.

Uislamu

Katika
Uislamu tohara hufundishwa kama wajibu wa kidini kwa kila mwanaume.
Hakuna amri katika
Kurani kuhusu tohara lakini inatazamiwa kama sunna ya mtume Muhamad. Kwa imani hiyo ni

ishara ya mitume ya kwamba walizaliwa bila govi katika hali ya kutahiriwa tayari.
Utekelezaji wa tohara huwa ni tofauti kati ya nchi na nchi; mara nyingi mtoto mdogo hutahiriwa kwa umri kati ya
miaka 5 hadi 10. Katika mazingira ya mjini wazazi wanawahi siku hizi kutahiri mapema.

Tohara kama hatua ya kiafya

Muda mrefu sana na nyembamba govi inaweza kuwa dalili za tohara matibabu

Siku hizi hata
mataifa yasiyokuwa na desturi hiyo yanaanza kuijali kwa sababu za usafi na afya.
Ni kwamba tohara inapunguza hatari ya mtoto kupatwa na
fimosis.
Imethibitishwa kuwa inapunguza uwezekano wa kuambukizwa
ukimwi pamoja na hatari ya magonjwa mengine kama kansa ya uume.
Katika nchi kadhaa sehemu kubwa ya watoto wa kiume wanatahiriwa mara baada ya kuzaliwa kwa sababu hizi za kiganga. Kwa mfano, huko Marekani asilimia 56 za wavulana wote waliozaliwa mwaka 2005 walitahiriwa katika hospitali walikozaliwa. Hata hivyo katika nchi hiyo kuna kampeni dhidi ya tohara kutokana na hoja ya kwamba mara nyingine upasuaji hauendi vizuri na kusababisha madhara ya kudumu kwa viungo vya uzazi.

Majibu:

1. Hakuna madhara ya kutahiriwa kama tohara itafanyika na daktari au ngariba mzuri. Uzuri wa tohara ni kuwa mwanaume anaweza kujiweka katika hali ya usafi kirahisi na kupunguza infection. Kichanga kufanyiwa tohara saa nyingine kunaweza kuuharibu uume wake kwa sababu bado mdogo na daktari anaweza kukata pasipo lakini huwa anapona haraka kuliko mtu mzima. Kufanyiwa tohara kienyeji (jando) kunaweza kuwa na athari zake. Naomba uangalie hii documentary (NOT X-rated) toka South Africa.

Ndiyindoda: I am a man - People & Power - Al Jazeera English

2. Hakuna madhara makubwa kwa mwanamke akifanya mapenzi na mume asietahiriwa hasa kama wako kwenye monogomous relationship. Kama mume ana wanawake wengi basi inakuwa rahisi kwake kusambaza magonjwa (kama yeast infection, nk.) kutoka mmoja hadi mwengine.

3. Ndio, mtu mzima anaweza kufanyiwa tohara. Baada ya kidonda kupona anaweza kuwa na sensitivity kidogo wakati wa kufanya mapenzi lakini hiyo itapita haraka sana. He will be back in full swing before he knows it.

4. Kwa mwanamke hataona tofauti yoyote katika utamu pre and post tohara ya mpenzi wake. Kwa mwanamme pia utamu utabaki palepale bali zingatia jibu na. 3.

I hope this helps.

Thank u Kifyatu kwa majibu yaliofungua ubongo wangu. Mungu akubariki sana kwa elimu unayotupatia thru JF. Hope wengi watafaidika na ushauri huu mzuri.
 
Back
Top Bottom