Mwandishi aliyewahi kupinga vita vya Ukreini awekewa Sumu

Mwandishi aliyewahi kupinga vita vya Ukreini awekewa Sumu

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Mwandishi wa habari kutokea Urusi Bi.Marina Ovsyannikova (45) ambaye alipata umaarufu baada ya kupinga vita ya Ukraine akiwa studio ameugua ghafla na inasadikiwa amewekewa sumu.

Marina alianza kufuatiliwa kimataifa mwezi Machi mwaka jana baada ya kuvamia studio ya televisheni ya taifa ya Urusi (alipokuwa amejiriwa) ,na kuingilia matangazo ya moja kwa moja akiishutumu Urusi kwa kuivamia Ukraine.

Mwandishi huyo alibeba bango lililoandikwa kwa lugha ya kirusi likimaanisha ”Sitisheni vita. Msiamini propaganda. Wanawadanganya hapa, Warusi dhidi ya vita”.

Polisi nchini Ufaransa wanafanya uchunguzi kuhusiana na uwezekano wa kulishwa sumu kwa Mwandishi huyo ambaye alikimbia Urusi na kuingia Ufaransa mwaka jana akiwa na binti yake.

Mwandishi huyo aliugua ghafla wakati akitoka nyumbani kwake jijini Paris, ndipo alipopiga nambari ya dharura ,kufuatwa na kupelekwa hospitali.

Mapema mwezi huu ,Mahakama jijini Moscow ilimhukumu Marina kifungo cha miaka nane na nusu jela (akiwa hayupo) kwa kusambaza taarifa za uongo kuhusiana na Jeshi la Urusi.

Pia kama umefuatilia mahojiano ya Yericko Nyerere kwenye channel ya Simulizi Na Sauti utagundua alisema kuwa ukiwa raia wa Urusi alafu ukaipinga Urusi au kuizodoa basi jiandae kutafutwa kijasusi popote Duniani na kuuliwa. Na Yericko Nyerere alinukuliwa akisema kwamba Urusi hakuna vikundi vya kigaidi kwa sababu ukiipinga serikali wewe adhabu yako ni kifo, hivyo Mwenye mamlaka ya kukuhukumu ni MUNGU lakini Putin ndio njia ya kukupeleka kwa huyo MUNGU kuhukumiwa. Kwamba wewe ni Mhaini hivyo mahakama zao haziwezi kupoteza muda kukuhukumu ni vyema putin akupeleke mbele za haki ukahukumiwe huko, kwa sababu ndiko mahali sahihi kwa kuhukumiwa watu kama hao.
 
Back
Top Bottom